HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 14, 2024

WOSIA UNAPUNGUZA MIGOGORO YA KIFAMILIA KWENYE URITHI WA MIRATHI

Mratibu wa Mradi Dkt. Albogast Msabilia



WATANZANIA wamekumbushwa umuhimu wa kuandika wosia na usimamizi wa mirathi ili kuepuka matatizo baada ya kifo chako.


Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa Ilvin Mugeta ametoa wito huo katika mhadhara Uliofanyika Chuo kikuu Mzumbe Morogoro china ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

"Kati ya watu 100 wanaofariki,hufa bila kuacha wosia, ijapokuwa wosia ni siri ni Muhimu unapoandika kuwa na madhahidi ili wajue kilichopo Kwenye wosia Ili kuepusha migogoro" amesema Jaji Mugeta.

"Kama unataka Mali zako ziwanufaishe watu wako unaowataka njia pekee ni kuacha wosia" ameongeza.

Amesema zipo baadhi imani na Mila potofu kuwa ukiandika wosia eti unajitabiria kifo, jambo ambalo Halina ukweli.

Aidha amesema kuna muhimu wa kupanga matumizi mali kwa kuandika Wosia ambao Utakuwa mwarobaini wa migogoro ya kifamilia ambayo imekua ikivunja amani na kuleta uadui

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi Dkt. Albogast Msabilia amesema kuwa, mradi huu umelenga kutekeleza katika sehemu saba ikiwemo kuhimarisha uhusiano baina ya chuo kikuu mzumbe na sekta binafsi pamoja na wadau wengine wakiwemo wananchi na wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad