HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 8, 2024

WAVAMIZI 130 WA ARDHI KIBAHA WAAMRIWA KUONDOKA KWA HIARI

Na Khadija Kalili Michuzi Tv
JUMLA ya Kaya 130 ambazo zimebainika kuwa walivamia eneo la Halmashauri ya Mji Kibaha ambalo linamilikiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Hati Miliki wametakiwa kuondoka mara moja kwa hiari yao katika eneo hilo la shamba namna 34,Pangani Kibaha Mji lenye ukubwa wa Hekta 1037 sawa na Ekari 2,592.5 ambalo linamilikiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa hati miliki.

Akizungumza leo January 8 katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri Mhandisi Mshamu Munde amesema

"Wananchi hao ambao wamevamia eneo hilo na kuliendeleza isivyo halali waanze kunusuru vifaa vyao vya ujenzi ambavyo wanaona vitawafaa katika makazi yao mapya tofauti na itakavyokuwa siku ambayo wataamua kubomoa kwani sheria ni msumeno"amesema .

Munde amesema kuwa tayari wameshakamilisha uhakiki wa eneo na kubaini wananachi ambao wamejenga ndani ya eneo isivyo halali huku akiwatoa hofu ya kuweza kununua viwanja kwa kufuata utaratibu na sheria za Halmashauri ya Kibaha Mji.

"Kiwanja namba 34 kilichopo Pangani Kibaha Mji ni sehemu ya eneo la ukubwa wa Hekta 4000 sawa na Ekari 10,000 ambalo lilitwaliwa kisheria na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kulipa fidia kwa wananchi waliokuwa wakimiliki eneo hilo kiasili, jumla ya wananchi 1556 walilipwa fidia yao kwa awamu nne kati ya mwaka 1988 na 1991.

Aidha Mkurugenzi Munde amesema kuwa hali halisi ya uvamizi katika eneo hilo la kiwanja namba 34 Kibaha ,baada ya Wizara ya Uvuvi kulipa fidia na kupima nakumilikishwa kiwanja hicho chenye ukubwa wa Hekta 1037,wananchi walivamia na kuuza sehemu ya kiwanja hicho na kujipatua fedha kwa njia ya udanganyifu na kufanya ujenzi kinyume na sheria,kwenye eneo ambalo tayari linamilikiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa hati miliki.

"Tayari wavamizi hao wa ardhi wameshapewa notisi ya kuondoka eneo la shamba hilo zaidi ya mara mbili ambapo awali aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa wakati huo Mh.William Lukuvi alifanya mkutano wa hadhara Julai 15,2021 katika Mtaa wa Lumumba ambapo pia ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Pwani,Uongozi wa Halmashauri ya Mji Kibaha pamoja na wananchi waliovamia kiwanja hicho.

"Katika mkutano huo alitoa maagizo kwa wananchi kuacha tabia ya kuvamia na kuuza eneo ambalo ni mali ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Ili kujiridhisha iliundwa Kamati ya kuchunguza uvamizi huo ambayo iliongozwa na Kamishna wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma pamoja na wataalam kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama ,Wataalam kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Pwani,Halmashauri ya Mji Kibaha na Wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ,Kamati hiyo ilipomaliza kazi yake iliwasilisha taarifa yake na mapendekezo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa wakati huo Mhe.Dkt.Angelina Mabula kwa pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa wakati huo Mhe.Mashimb Ndaki na haya yote yalielezwa katika mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Septemba 2,2022 katika Mtaa wa Lumumba Kata ya Pangani .

"Halmashauri ya Mji Kibaha ilitoa notisi ya kwanza Novemba ,22 ,2022 na Oktoba 14, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge alifanya mkutano wa hadhara katika eneo hilo na kutoa siku 60 kwa wananchi waliovamia eneo hilo kuondoka mara moja huku akiwasihi wabomoe nyumba zao wao wenyewe ili kuweza kunusuru vifaa vya ujenzi ambavyo vitawasaidia baadaye.

Aidha RC Kunenge aliagiza mamalaka ya upangaji kwa kushirikiana na mmiliki wa Kiwanja namba 34 Pangani kupanga upya na kupima eneo hilo kwa kuzingatia mahitaji ya mmiliki na Taasisi zake pamoja na Taasisi nyingine za serikali ya Halmashauri ya Mji Kibaha huku akisisitiza watu wote ambao waliojihusisha na uuzaji ardhi kwa njia ya utapeli wafikishwe kwenye vyombo vya sheria, hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya viongozi wa Mitaa,Watendaji wa mitaa pamoja na wataalamu waliohusika katika kusaini na kupitisha mauziano ya ardhi katika shamba namba 34 Pangani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad