HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 31, 2024

UBALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA WAPONGEZWA UTOAJI ELIMU USALAMA BARABARANI DODOMA

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

UBALOZI wa Uswisi nchini Tanzania umepongezwa na madereva bodaboda jijini Dodoma kwa kufadhili mafunzo ya usalama barabarani ambayo yametolewa na Shirika la Amend Tanzania.

Shirika la Amend kupitia ufadhili wa ubalozi huo liliendesha mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva bodaboda zaidi ya 250 ambapo kwa sasa bodaboda hao wamekuwa mabalozi wa elimu hiyo kwa wengine ambao hawakuipata wakati wa mafunzo hayo.

Akizungumza jijini Dodoma Balozi wa Mafunzo ya Usalama Barabarani ambaye pia ni dereva bodaboda eneo la UDOM Nuhu Toyi ameeleza kwa kiasi kikubwa wanaushukuru wa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania kwa kuona haja ya kutoa mafunzo hayo kwa kuliwezesha Shirika la Amend kuwafikia madereva bodaboda wa Jiji la Dodoma.

“Pongezi za dhati ziende kwa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania hususan kitengo cha afya kinachofadhiliwa na miss Vivian kwa kutambua umuhimu wa kundi hili la vijana wa bodaboda wengi ni vijana ambao tupo kati ya umri wa miaka 25.

"Tumekuwa tukiifanya kwa mazoea na hatuna elimu kwahiyo wengi tumekuwa ni waathirika wa kusababisha au kusababishiwa ajali kwasababu ya kukosa elimu barabarani lakini ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania umeona itakuwa ni vyema kama vijana hawa ambao ni taifa la kesho na nguvu kazi ya taifa wasiweze kudhuulika na ajali."

Kwa upande wake dereva bodaboda Laurenti Mayowa amesema alikuwa haelewi alama za barabarani lakini kupitia mafunzo hayo wamepokea kutoka shirika la Amend Tanzania sasa wameelewa kwani wamefundishwa kwa nadharia pamoja na vitendo.

“Tulipata mafunzo mazuri sana kwenye swala la uendeshaji wa pikipiki lakini pia tumeweza kufundishwa namna ya kutumia barabara lakini pia namba ya kutumi vyombo vyetu, kwa kweli mafunzo yalikuwa mazuri ...

"Nimejifunza mambo mengi na mazuri na kabla ya mafunzo nilikuwa sielewi kwamba barabarani nilikuwa naendesha hovyo hovyo tu na baada ya mafunzo nashukuru mpaka sasaivi nime elewa na tulikuwa wengi sana tukifundishwa awamu kwa awamu nafikiri bodaboda takriban 230 au 250 kwa Dodoma hapa na sasahivi wame elimika”, amesema Mayowa.

Ameongeza alama za barabarani ilikuwa ni changamoto kwa madereva wengi , walikuwa wanaziona lakini wanashindwa kuzitumia kama ipasavyo na walidhani ni michoro tu lakini baada ya mafunzo waliweza kuelewa aina za michoro na alama zinazotumiwa barabarani.

“Tulifundishwa kuna alama za onyo, alama za amri, kuna alama za maelekezo kwahiyo yote haya tumefundishwa pia nimefundishwa alama nyengine ambazo nilikuwa sizielewi vizuri kama alama za michoro juu ya sakafu ya barabara hizo nazo nilikuwa sizielewi nilikuwa naona tu michoro na sielewi maana yake na baada ya elimu nimeelewa vizuri” amesema Mayowa

Aidha amesisitiza kwa maafisa usafirishaji kubadilika na kuwa na mahudhurio mazuri ya mafunzo yanayotolewa na shirika la AMEND Tanzania kwasababu yanafundishwa kwa vitendo pamoja na kutii sheria za barabarani.

“Tumefundishwa dereva kujihami kwahiyo wale ambao hawajapata mafunzo hawawezi kuelewa na kutii sheria akiwepo barabarani na anaweza kusababisha ajari kwasababu anakuwa hana uelewa wowote lakini vigumu kujilinda anapotumia chombo chake”,Mayowa.

Wakati huo huo dereva bodaboda Ally Rashid Ally amesema uendeshaji bodaboda ni ajira kama zilivyo ajira nyengine na imeteka soko kubwa la ajira kwa vijana kwenye upataji wa kipato na awali haikupewa thamani kama zilivyo biashara nyingine.

Amesema wamekuwa na madereva usafirishaji wengi lakini baadhi yao kwenye kundi hilo hawana elimu ya kutosha ya barabarani na kutambua alama zilizomo, hivyo elimu iliyotewa ni msaada mkubwa kwa maofisa usafirishaji mkoani Dodoma .

"Kwasasa wengi wao wamekuwa na nidhamu iwapo wanatumia vyombo vyao barabarani na changamoto za ajari na vifo vimeweza kuepukika kutokana na maarifa waliopokea kutoka kwa wakufunzi kupitia shirika la Amend Tanzania."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad