Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Msomera, Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Na Khadija Kalili, MSOMERA
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO ,
Mobhare Matinyi amesema kuwa wataalamu wa masuala ya ekolojia wameiambia Serikali kuwa endapo hawatasimamia kidete suala la kuwahamisha wananchi wanaoishi katika hifadhi ya Ngorongoro itapotea ifikapo 2050 ikiwa ni pamoja na wanyama kutoweka kabisa.
Matinyi amesema hayo leo alipokua akizungumza na waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari ambao wamefanya ziara kwenye hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ambapo wamejionea namna wananchi wanavyoishi na mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo na baada ya hapo wametembelea makazi mapya ya Msomera yanayojengwa na serikali.
Matinyi amesisitiza kuwa serikali bado inaendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo huku idadi kubwa wakiendelea kujiandikisha kuhama.
"Awali idadi ya wakazi waliokuwa wakiishi ndani ya hifadhi ilikua chache ambao ni 8,000 ambao pia walikua na mifugo michache tofauti na ilivyo sasa ndani ya hifadhi kumekua na kaya 100,000 huku mifugo ya ng'ombe, mbuzi, kondoo wamezidi kuzaliana hali ambayo imesababisha kuwakimbiza wanyama wa asili.
'Hivyo basi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haitakuwa tayari kuipoteza Ngorongoro ndiyo maana tunaendelea kuwahamisha wakazi kwa kuwalipa fidia na kuwajengea nyumba. "
"Serikali inatoa elimu ya uhamasishaji inafanya tathmini ya kuwalipa kila mtu mwenye mali anayomiliki ambao wanaishi katika hifadhi ya Ngorongoro na baada ya kuwalipa kwa kila kaya ikiwa ni pamoja na kupewa kiasi cha fedha cha Milioni 10, huku mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro itamhamisha kwa gharama zake bila kulipishwa muhusika yeye, mali zake ikiwemo mifugo pamoja na familia yake kwenda kwenye makazi mapya yaliyopo Msomera Wilaya Handeni Mkoani Tanga.
"Tayari zimeshafanyika awamu mbili huku ya kwanza imefanyika 2022 sasa tupo kwenye utekelezaji awamu ya pili ambayo imeanza Julai 2023 na inatarajiwa kukamilika Machi , 2024 huku lengo kubwa la serikali ni kujenga nyumba 5,000 katika eneo linalojumuisha Kitwai, Sauni na Msomera kwa ajili ya wakazi wa Ngorongoro wanaohamia kwa hiyari eneo la Msomera."
Amesema Matinyi.
Matinyi amesema kuwa kila mwananchi anajengewa nyumba yenye vyumba vitatu anapewa fursa ya kuunganishiwa umeme na TANESCO kwa gharama ya 27,000, huku Wizara ya Maji inachimba visima ambavyo vitakuwa na sehemu za kusambazia maji ili wananchi waweze kupata maji.
Matinyi amesema kuwa kwa upande wa wananchi ambao hawatopenda kuhamia Msomera watapewa fidia ya mali zao, watasafirishwa kwa gharama ya serikali hadi katika Mkoa ambao wameuchagua nakupewa kiasi cha Sh. MI.15 tu.
"Kuna Wizara tayari zimefika hapa Msomera zikaunda timu ya pamoja ili kufanya oparesheni hii ifanikiwe zipo Wizara kumi ambazo ni Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Maliasili na Utalii, Nishati, Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kilimo, Maji, Mifugo na Uvuvi, Maendeleo.
Aidha Matinyi amesema kuwa Wizara ya kilimo imesema mbali ya kuwatengea mashamba wameanzisha mashamba darasa kwa wakazi hao ili wananchi hawa waweze kulima mbali na shughuli walizokuwa wamezizoea awali za ufugaji.
Akifafanua kuhusu shughuli za kiuchumi amesema kuwa zinakwenda kuongezwa ili maisha ya wananchi hao yawe mazuri.
"Milango iko wazi kwa wawekezaji waje kuwekeza katika mji huu mpya na wa kisasa amesema Matinyi.
"Kutajengwa minada ya kisasa ili wananchi wapate nafasi ya kupanua ukuaji wa wigo wa uchumi, kujenga vituo vya kukusanyia maziwa, kwani wafugaji ukiacha uuzaji wa nyama kwenye mnada huwa wanauza maziwa kwa hiyo kutakuwa na vituo kwa ajili ya wananchi kupeleka maziwa na kupata pesa." Amesema Matinyi
Wakati huohuo Msemaji Mkuu wa Serikali Matinyi ametoa wito kwa Asasi za Kiraia pamoja na vyombo vya nje ya nchi kuacha kutoa taarifa za mbaya na za uongo kuwa uhamishwajiwa wananchi unakiuka haki za binadamu.
"Hizi ni propaganda za watu wachache mbao wanania ovu hivyo ili waweze kujiridhisha tunawakaribishawaje Ngorongoro na Msomera ili kuona hali halisi ya maisha walikokua wakiishi kabla na baada kisha ndipo waende wakaitangazie dunia.
"Serikali haiko tayari kuona wananchi wake wanaishi katika mazingira hatarishi na wanyama wakali ambao wamekuwa wakiwasababishia maafa ikiwemo vifo ikiwemo kutoishi kwa uhuru wa kutembea kwani ndani ya hifadhi mwisho wa kutembea nisaa 12 jioni.
No comments:
Post a Comment