HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 26, 2024

TRA YAWATAMBUA WADAU WAKE

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata akitoa tuzo leo Januari 26, 2024 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo imepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata amepongeza juhudi zinazofanywa na forodha na wadau mbali mbali katika ukusanyaji wa kodi unaopelelekea kukuza uchumi wa nchi.

Kidata amesema hayo leo Januari 26,2024 jijini Dar Es Salaam wakati akkikabidhi tuzo za sifa kwa wadau wa TRA ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Forodha Duniani ambayo huazimishwa kila Mwaka Januari 26.

Amesema maadhimisho hayo yalianzishwa tangu mwaka 1964 kwa lengo la kutoa tuzo za  sifa kwa wadau wa forodha.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Forodha wa TRA, Juma Hassan amesema maadhimisho hayo ni kudhihirisha kwa umma kazi zinazofanywa na forodha kwa kushirikiana na wadau.

"Jukumu la msingi la forodha ni kurahisisha biashara lakini pia kutekeleza majukumu kuhakikisha watu wanalipa kodi kabla ya kuingiza mzigo, kuwatambua wadau wote na kazi wanazofanya, kuwatambua washirika wa zamani na wapya na taasisi kutoa miongozo ya bidhaa zinazoingia nchini,”amesema Hassan.

Amesema wao kama forodha jukumu lao ni kukagua mzigo kushirikiana na taasisi zote zinazofanya kazi kwa pamoja hivyo wameanzisha mfumo wa ‘single window’ na taasisi zote zinafanyaka kazi kwa mfumo huo mmoja kuondoa vikwazo kwa walipa kodi.

Aidha amesema wameongeza  ushirikiano kwa sababu forodha yenyewe haiwezi kutimiza majukumu hayo bila kushirikiana na Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) na taasisi zinazohusika.

“Kuendelea kuboresha mifumo na kuongeza ufanisi, ubunifu katika kazi zetu kwa weledi,” amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema uchumi wa Tanzania unakua kupitia forodha kwa kusimamia sheria za forodha duniani na nchini.

Ametoa wito kwa wadau wote wanaohusika kna uchumi kuendelea kulipa kodi stahiki za serikali na kuhakikisha hawakwepi kodi na kuwa wazalendo katika nchi yao.

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maaluumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema ni siku muhimu ya forodha duniani kwa mfanyabiashara mdogo, kati na mkubwa.

Amesema wataendelea kuimarisha usalama maeneo mbalimbali kwa kuwa ni wajibu wao kama Jeshi la Polisi
 
"Kila mtanzania ajue thamani ya kulipa kodi kwani watu wengi wanafikra za kupata nafuu ya bei kwenye bidhaa mbalimbali kwa kutokulipa kodi, kwa kufanya hiyo kunasababisha kutokuwepo na huduma bora. Katika jamii." Amesema

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 26, 2024 mara baada ya maadhimisho ya siku ya Forodha duniani.
Kaimu Kamishna wa Forodha wa TRA, Juma Hassan akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 26, 2024 mara baada ya maadhimisho ya siku ya Forodha duniani.


Baadhi ya washiriki Wakati TRA wanaadhimisha siku ya forodha duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad