HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 23, 2024

SERIKALI YAONDOA ZAIDI YA TOZO 374 KUWEZESHA SEKTA BINAFSI KUFANYA KAZI KWA UFANISI

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida,amesema kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI) umeweza kupunguza na kuondoa zaidi ya tozo 374 na kurekebisha zaidi ya Sheria na Kanuni 55 zinazowezesha Sekta binasfi kufanya kazi kwa ufanisi.  

Hayo yameelezwa Januari 22, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kida amesema kuwa Tozo zilizoondolewa au kupunguzwa na Sheria na Kanuni zilizorekebishwa zimelenga Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji  katika sekta za Uwekezaji, Kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, Utalii, Nishati, Madini, viwanda na Biashara

Aidha, Dkt. Kida amesema kuwa Mradi huo umelenga katika kukuza uchumi, kuongeza ajira na ubunifu kwa vijana na wanawake, kwa kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji pia kuongeza usalama wa mlaji na kuwezesha wajasiriamali wakubwa, wa kati na wadogo kuzingatia ubora wa Bidhaa.

Dkt. Kida amefafanua kuwa, Mradi huo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), umetoa jumla ya Euro milioni 23 sawa na fedha za kitanzania Bilioni 63.5 ambazo  zimeelekezwa kufadhili miradi  mitatu  ikiwemo Mpango wa Kuboresha  Mazingira ya Biashara na Uwekezaji  (MKUMBI) ambao awali ilikua ikijulikana kama BLUEPRINT.   Vilevile amefafanua kuwa  fedha hizi zimelekezwa katika Mradi wa QUALITAN uliojikita  kuimarisha maabara za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na  mradi wa FUNGUO unatekelezwa na UNDP ambao umejielekeza katika kuwawezesha kampuni changa zinazochipukia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mahusiano wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw.  Cedric Merel amesema  Kamati imejadili  kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara nchini na jinsi ya kusaidia kampuni zinazoibukia kukua na kuyafikia masoko. 

Naye  Mkuu anayesimamia Masuala ya UNIDO Bara la Afrika Bw. Victor Djemba wanaendelea kusisitiza wazalishaji kuzingatia ubora ili  kuyafikia masoko makubwa na amehaidi kuendelea kushirikiana na Umoja huo ili kufikia malengo   yaliyowekwa.
Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida akisisitiza jambo wakati akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.
Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mahusiano wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Cedric Merel akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, Bw.Shigeki Komatsubara akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP,  Bw.Shigeki Komatsubara akiwa katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Prof. Mkumbukwa Mtambo akiwa katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.


Wadau wa Uwekezaji nchini wakiwa katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa uwekezaji na viwanda wakati wa Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad