HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 22, 2024

MAWASILIANO YA UNUNIO MBUYUNI YAREJEA, TANROADS WAPEWA MAAGIZO

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea miundombinu ya barabara iliyoharibika katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Viongozi mbalimbali wakiangalia Daraja la Mto Tegeta katika barabara ya Mbuyuni, Mtongani, Ununio Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya huduma kurejea tena ikiwa maji ya mvua yalikata tuta la barabara wakati wa Mvua zilizonyesha Januari 20, 2024.

Jangani Usafi ukiendelea baada ya tope kuwepo barabarani.
Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 22, 2024 wakati wa ziara ya kutembelea miundombinu ya barabara iliyoharibika.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya amewaagiza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wameaswa kuwa na mpango wa Muda mrefu wa kutengenezea maji njia sahihi ili yasiweze kubomoa Madaraja.

Hayo ameyasema leo Januari 22, 2024 wakati wa ziara na waandishi wa habari ya kutembelea barabara zilizoharibika pamoja na barabara zisizopitika kwa urahisi, ziara hiyo iliambatana na Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga pamoja, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule pamoja na Wafanyakazi wa TANROADS. Amesema licha ya Daraja la Mtongani katika mto Tegeta kukupitika wahakikishe wanafungua barabara hiyo upande mwingine ili huduma ziwe kama kawaida.

 “Muwe na mipago ya muda mrefu kuangalia kama je! Daraja hilo linatosheleza kama halitoshelezi iangaliwe namna na kama makalavati hayatoshelezi basi mjenge daraja au kutafuta namna nyingine ya kingo sahihi ambazo maji hayatakata barabara.”

TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam amewaomba kukagua maeneo yote ya madaraja na wanapoona kunachangamoto yeyote inatokea ili kuokoa maisha ya vyombo na maisha ya watu kuwa na haraka ya kutoa alama za kuonesha kuwa mahali hapapitiki au kunahatari ili watu waende kwa tahadhari.

“Tusione shida kuweka alama za tahadhari ili kuokoa maisha ya watu yanapokuwa hatarini.” Ameeleza

Kwa upande wa wananchi amewaasa kutekeleza maelekezo wanayopewa na wataalamu kwaajili ya usalama wao na maisha kwa ujumla.
Licha ya hayo amewashukuru wakandarasi kwa kuwa tayari kurejesha mawasiliano katika eneo la mto Tegeta katika barabara ya Mbuyuni, Mtongani na Ununio.

Kwa Upande wa Mkuu wa Kitengo cha matengenezo TANROADS Dar es Salaam, Mhandisi Suzana Lucas amesema kuwa ndani ya masaa 48 wamehakikisha barabara ya Mbuyuni Kunduchi na Ununio inafunguliwa kutokana na kuharibika mvua zilizonyesha Januari 20, 2024 jijini Dar Es Salaam.

“Hii kazi tumefanya usiku na mchana mpaka sasa barabara imeweza kufunguliwa upande mmoja kutokana na hali ilivyokuwa mwanzo, athari hizi katika barabara Mbuyuni Ununio maji yalianzisha njia nyingine na kusababisha udongo kuondoka kwahiyo tuliweka mawe na kuweka zege kazi kubwa ni kuelekeza maji yarudi kwenye mkondo wake na kwa sasa maji yanapita darajani, zile mvua zilisababisha maji kubadilisha uelekeo na kula tuta la barabara.” Amesema Mhandisi Suzan

Pia amesema katika kurejesha huduma ya barabara walitoa takataka zilizokuwa zimeziba midomo ya daraja na kwa sasa maji yanapita vizuri kwenye daraja.

Kwa Upande wa Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amewashukuru wafanyakazi wa TANROAD pamoja na Wakala wa barabara za mji na Vijijini (TARURA) kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kurudisha mawasiliano katika barabara ya Mbuyuni Ununio katika daraja la Mtongani, Daraja la Mpiji, Mbweni JKT na madaraja mengine madogo ya Mbopo na Msumi na la barabara ya Tanganyika.

Amesema madaraja hayajaharibika bali ni barabara zilizokatika na kubakisha Madaraja.

Pia ametoa wito kwa wananchi wakati mvua zinaendelea kunyesha kuchukua tahadhari wakati wa kupita kwenye barabara mbalimbali za Dar es Salaam maji yakiwa yanapita kwa wingi kwenye mitaro na kama ardhi haionekani ni vyema kusubiri maji yapite ndio upite.

“Tusipite maeneo ambayo maji yapo juu ya ardhi bila kujua chini kuna mazingira gani.”

“Wilaya yetu Kinondoni tumejitahidi kusafisha mitaro yote inayopitisha maji ya mvua ndio maana mvua ikinyesha ndani ya masaa mawili baada ya mvua maji yote yanakuwa yameshaelekea baharini.” Amesema Dc Mtambule

Pia Dc Mtambule ametoa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu ambao bado haujafika katika mkoa wa Dar es Salaam kufuata maelekezo ya wataalamu yaliyotolewa ili ugonjwa huo usifike.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad