HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 22, 2024

MAKAMISHNA WA KODI JUMIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

 

Katibu Mkuu, Wizara ya fedha, Dkt. Natu Mwamba akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari mara baada ya kufungua mkutano wa 51 wa Makamishna wakuu wa Mamlaka za Mapato Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Jumla ya nchi sita zinashiriki mkutano huo.

Katibu Mkuu, Wizara ya fedha Dkt. Natu Mwamba akizungumza na makamishna wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati  akifufungua mkutano wa 51 wa Makamishana wakuu wa Mamlaka za Mapato Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Jumla ya nchi sita zinashiriki mkutano huo
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA) John Musinguzi akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa mkutano wa 51 wa Makamishna wakuu wa Mamlaka za Mapato Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Jumla ya nchi sita zinashiriki mkutano huo wa siku mbili unaendelea jijini Dar es Salaam na utafikia Tamati kesho Januari 23,2024.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini,  (TRA) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari leo Januari 22, 2023 wakati wa mkutano wa 51 wa Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Jumla ya nchi sita zinashiriki mkutano huo unaoendelea jijini Dar es Salaam.


KAMISHNA wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki,  wamekutana kwa ajili kujadili mambo mbalimbali ikiwemo sera na sheria za kodi zinazokinzana katika nchi hizo ili zifanyiwe marekebisho.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa 51 unaofanyika jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema kila mwaka nchi hizo hukutana mara mbili wakiwa na mitaala mbali mbali ambayo inangalia sera na sheria za kodi.

“Kwa sababu lengo kuu la nchi ni kuwa na soko la pamoja ambapo tunafanya biashara kwa pamoja, tunategemeana kwa mengi, kwa hiyo kunapokuwa na sera ambayo inaleta shida tunaizungumza, tunaiweka vizuri ili isiwe kikwazo katika ufanyaji wa shughuli za kibiashara katika nchi zetu.

“Lakini pia kama kuna sheria ya kodi ambayo inakinzana na sheria ya nchi nyingine na yenyewe tunaipitia basi tunaiweka pamoja,” alisema.

Amesema kwa kuwa wanakutana nchi mbalimbali, maendeleo ya teknolojia katika nchi hizo yapo tofauti kwa hiyo wanaangalia eneo la teknolojia kwa nchi ambayo imepiga hatua ili wamfuate kwa kuwa soko lao ni moja.

Pia ametaja eneo lingine ni la magendo ambalo limekuwa likiathiri nchi hizo, hivyo wanashirikiana kwa kusaidiana kutoa taarifa na kufanya uperesheni pamoja.

“Lakini pia tunakuwa na msimamo wa pamoja katika masuala ya kimataifa ambayo tunatetea maslahi yetu kwa pamoja kama jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA), John Musinguzi amesema mkutano huo ni mzuri kwa kuwa wanabadilishana taarifa, uzoefu na teknolojia, pia wanashirikiana kwenye mipaka, vitendea kazi na miundombinu.

“Tunapokutana tunajaribu kuweka sawa maeneo yenye changamoto,” amesema.

Naye,  Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba amesema mkutano huo ni muhimu kwa sababu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, makamishna wa kodi wamekutana kwa pamoja, maana yake ni kwamba watazungumza mambo yanayoweza kuleta ufanisi zaidi ya yale ambayo yanakuwa vikwazo.

“Nimeambiwa watazungumzia mifumo ya kukusanya mapato ni muhimu sana na lazima isomane katika nchi zetu tofauti, na pia sisi kwa kuwa tunashirikiana, kwenye mipaka ni muhimu sana kuona kodi zinachukuliwaje,” alisema.

Makamishna walioshiriki ni kutoka nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad