HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 24, 2024

KITUO CHA MAFUTA CHA VICTORIA KUTOA HUDUMA YA BIDHAA ZA CASTROL

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMPUNI ya usambazaji wa mafuta na vialinishi vya Castrol nchini, Wambi Lube wamezindua huduma ya Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria ambapo kitaweza kusaidia wateja kupata huduma ya vilainishi na sehemu maalum ya kusubiri huduma yenye huduma za michezo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24,2024 Jijini Dar es Salaam, mwakilishi kutoka kwa Castrol Makao Makuu na Meneja wa Afrika Mashariki Bw Ed Savage amesema kuwa wateja wanaweza kupata huduma ya Castrol za daraja la kipekee na pia uhakika wa upatikanaji wa mafundi na wahudumu wa duka walioelimishwa.

Aidha amesema kuwa huduma hiyo inalenga kuhakikisha wateja wa bidhaa za Castrol kuendelea kupata bidhaa bora yenye kupendekezwa kutumika na watengenezaji magari mahiri wanaongoza duniani ili kuhakikisha upatikanaji wa vilainishi halisi vya Castrol 100%.

Na Meneja wa Mauzo wa kampuni ya Wambi Lube, Bw. Steven Jonathan amesema kwasasa ukishafika katika kituo cha mafuta cha Victoria utakutana na mafundi ambao wamefundishwa kuhusu bidhaa za castrol.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kituo cha Mafuta Cha Victoria Bw. Renald Kyando amesema watumiaji wengi wa magari wamekuwa wakipendekezwa kutumia bidhaa za Castrol wakati wakitaka kubadili vilainishi kwenye magari yao, hivyo basi kituo hicho cha mafuta watakuwa wanatoa huduma bora kwa wateja wao kupitia bidhaa za Castrol ambazo ni bora na za kuaminika.

Amesema kupitia uzinduzi wa huduma hiyo, watahakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wale ambao watahitaji bidhaa za castrol hasa vilainishi ambavyo watakwenda kuvitumia kwenye magari yao

.
Mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Victoria Bw. Harold Matemba (katikati) akipokea cheti cha uwakala wa uuzaji wa vilainishi vya Castrol Oil hapa Tanzania kutoka kwa Meneja wa Afrika Mashariki Bw Ed Savage wakati wa uzinduzi wa huduma za Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria leo Januari 24,2024 Jijini Dar es Salaam


Mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Victoria Bw. Harold Matemba (katikati) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Meneja wa Afrika Mashariki Bw Ed Savage wakati wa uzinduzi wa huduma za Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria leo Januari 24,2024 Jijini Dar es SalaamUzinduzi wa huduma za Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria uliofanyika leo Januari 24,2024 Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad