HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 26, 2024

KAMPENI YA "MPE MAUA, ATABASAMU ASOME KIFALME" YAZINDULIWA MANYARA

  

Na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG

Mirerani, Simanjiro 26 Januari 2024: Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amezindua kampeni iliyopewa jina la "MPE MAUA, ATABASAMU ASOME KIFALME" katika eneo la Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro.

"Mpe Maua Atabasamu asome Kifalme" ni Kampeni inayolenga kuboresha sekta ya Elimu Kama ambavyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inavyofanya maboresho makubwa katika sekta hiyo kwa kujenga na kurekebisha miundombinu.

Akizungumza wakati akizindua kampeni hiyo, Mhe. Sendiga amesema kuwa kwa sasa shule nyingi bado zinakabiliwa na changamoto ya madawati, hivyo kupitia kampeni hii wataweza kushirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuweza kufanikisha zoezi hilo na kwa haraka. "Nimewaita leo ili kuwaomba wadau na wazawa wote wa Mkoa wa Manyara kuja kuungana nasi kuwapa watoto tabasamu kwa kuwawezesha kusoma katika mazingira yanayovutia", amesema Mhe. Sendiga.

Vilevile Mhe. RC amesema kuwa matarajio ya kampeni hiyo ni kuhakikisha vinapatikana viti na meza 4,664 na madawati 28,336 ili kuweza kukidhi mahitaji ya mkoa kwa ujumla.

Aidha, RC Sendiga amewaasa wazazi na walezi kuendelea kuwalea watoto katika maadili mema ili kuwaepusha na mambo maovu.

Katika kipindi cha uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan mkoa wa Manyara tumeweza kupokea fedha takribani bilioni 91.4 katika sekta ya Elimu, fedha hizo zimetumika kwenye kutengeneza na kurekebisha miundombinu ya shule.

Mwisho amewashukuru wadau ambao ni wachimbaji wa madini ya Tanzanite ambayo ni Kampuni ya FRANONE, Kiria Laizer na Wazazi kwa kuunga mkono kampeni hiyo kwa kuwapa Maua ya upendo Watoto wa Manyara kwa kuchangia jumla ya madawati 142.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad