HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 19, 2024

betPawa yanogesha Afcon kwa kumwaga zawadi kwa mashabiki Dar

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya betPawa imenogesha fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Ivory Coast kwa kumwaga zawadi mbalimbali kwa mashabiki.

Kampuni hiyo kwa sasa inaendesha kampeni “Soka Live na betPawa” ambapo mbali ya kuwakutanisha mashabiki kuangalia mpira pamoja, pia uwazawadia zawadi mbalimbali kama jezi, mabegi, mipira, vikombe, chupa za maji na nyingine kemkem.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulianyika kwenye baa ya Kitambaa Cheupe, Sinza ambapo mashabiki walipata fursa ya kuangalia ‘live’ mechi ya kwanza ya timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars ambayo ilipoteza dhidi ya Morocco kwa kufungwa mabao 3-0.

“Soka ni mchezo unaounganisha na furaha na hasa pale mashabiki wanapojumuika pamoja. Hii ndiyo sababu tuliona inafaa kwa betPawa kwa kushirikiana na Startimes kuendesha kampeni hii ili kuwafanya mashabiki kuishangilia Taifa Stars wakiwa na ari moja,”alisema Meneja Masoko wa betPawa nchini Borah Ndanyungu.

Mashabiki hao pia walipata kujumuika na timu za betPawa na Startimes zilizokuwapo kujibu maswali yao kuhusu huduma za burudani zinazotolewa na kampuni hizo mbili.

Zaidi ya watu 300 walihudhuria hafla hiyo ambayo pia iliambatana na muziki mzuri na burudani mbalimbali.

"Matukio haya ya kutazama mechi pia yatatusaidia kukutana na wateja kwa urahisi wao kama sehemu ya ahadi yetu ya utoaji wa huduma," alisema Ndanyungu.

Alisema kuwa kampeni hiyo itaendekea Jumapili Januari 21, 2024 wakati Taifa Stars itakapokuwa inapambana na Zambia. Hafla hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Juliana Pub pale Mbezi Beach kuanzia saa 6.00 mchana.

Mashabiki wakipokea zawadi ya fulana kutoka kampuni ya michezo ya kubahatisha ya betPawa

 

Mashabiki wakiangalia ‘live’ mechi ya Afcon kati ya Taifa Stars dhidi ya Morocco kwenye ukumbi wa Kitambaa Cheupe Sinza kupitia kampeni ya Soka Live na betPawa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad