HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 16, 2024

BASATA YAHAIDI KUMSHIKA MKONO MADAM RITA

 

BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) Lakiri kuguswa na juhudi zinazofanywa na Madam Rita kupitia shindano la Bongo star search (BSS) Kwa kuzalisha na kunyanyua vipaji vya vijana wengi nchini kupitia Fani ya Muziki.

Akizungumza hayo wakati wa kutangazwa kwa fainali ya Shindano hilo mapema Leo Januari 16,2024 Afisa Mwandamizi (BASATA) Agustino Makame amesema Baraza linatambua mchango mkubwa unaofanywa na Shindano hilo katika kufufua,kukuza na kuwapa nafasi ya kutumia Jukwaa hilo kutimiza ndoto za Vijana wengi na hivyo kama Basata litakaa chini kuendelea kutoa ushirikiano kw Waandaaji hao.

Hata hivyo Makame amesema Waandaaji hao wamekuwa wakishirikiana na Basata tangu kuanza kwa mchakato wa awali hadi kuelekea kwa Fainali hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Startimes David Malisa amesema msimu huo wa 14 ulikuwa wa kitofauti kutokana na timu hiyo kufika Mji wa Kigoma na kupata writhing wengine wa Peter Msechu.

Aidha amesema wao Kama Startimes wataendelea kuunga Mkono Jitihada za Mama huyo kwa kuona ipo haja ya Jukwaa la BSS kutumika kwa Vijana hata walio Mikoani na kuwafikia kwa Lengo la kutimiza ndoto zao kupitia Muziki.

Pia Malisa amesema Fainali hizo zitarushwa mubashara kupitia St Swahili bila chenga ili kuwapa fursa ya kuwaona burudani mbalimbali usiku wa Kilele cha Fainali hizo.

''Kiingilio cha kawaida sh 15000, VIP 30,000 na VVVIP ni sh 50000. Hivyo kwa wale ambao hawajajiunga na familia ya Startimes wajiunge sasa ili wapate kushuhudia kila kitu,"

Kwa upande wake Jaji mkuu wa shindano hilo Rita Paulsen ameeleza utofauti wa Msimu wa 14 wa shindano hilo sababu kubwa akieleza kuwa vipaji vimekuwa vingi vizuri tofauti na misimu iliyopita na kulazimika fainali kusindikizwa na sita bora (Top 06) baadala ya tano bora (Top 05) kama ilivyozoeleka.

"Msimu wa 14 vijana wamejitokeza wengi na mikoa mengine ilitulazimu tuchukue watu wengi na baadae tulipofanya mchujo tumebaki na na Vijana 06 ambao wamefanikiwa kuingia kwenye mchakato wa ushindani."

Hata hivyo Paulsen ameweka wazi kuwa zawadi ya Mshindi wa kwanza atapewa Kiwanja pamoja na pesa taslimu milioni 20,wakati mshindi wa pili atapewa milioni 3 huku washindi waliobakia wakipatiwa kifuta jasho milioni 1 kila mmoja.

Pia ametoa wito kwa wizara husika pamoja na Baraza la sanaa Taifa (BASATA) kuweka nguvu kubwa kuwasaidia Waandaaji wa Bongo star search (BSS) Kutafuta wadau watakaoongeza nguvu kubwa kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa ufanisi mkubwa zaidi.

"Kiukweli tunahitaji nguvu kubwa mno katika shindano hili bado tunahitaji wadau tunaomba wizara husika watupe nguvu na waombe udhamini kwa Taasisi na Wizara mfano Wizara ya Utalii Inakuwa rahisi wenyewe kwa wenyewe wizara za serikali kusikilizana kwa haraka na kupatikana majibu kwa wepesi zaidi."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad