HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 9, 2023

TOYOTA CROWN YAWAWEKA ROHO JUU WASHIRIKI WA BINGWA

 

IKIWA zimebaki siku kadhaa kuelekea Fainali ya Shindano la Bingwa Kampuni ya StarTimes Media imetambulisha zawadi ya gari aina ya Toyota crown yenye thamani ya Sh milioni 20 itakayotoa kwa mshindi wa shindano la bingwa msimu wa pili katika fainali itakayofanyika wiki ijayo.

Shindano la bingwa msimu wa pili lilizinduliwa tangu Julai mwaka huu na kushirikisha washiriki 24 ambao ni maarufu mitandaoni waliokaa katika jumba moja maalum kuonesha uhalisia wa maisha yao na kuoneshwa kwenye televisheni ya Tv3.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes, David Malisa alisema mshindi wa jumla sio tu ataondoka na gari bali fedha taslimu ambazo itakuwa ni kama ‘surprise’ zitakazoenda kumsaidia kuendesha maisha yake.

“Tunawashukuru Watanzania wanaoendelea kufuatilia vipindi vyetu, msimu huu wa sikukuu tunawaambia Lipa Tukubusti, lipia vifurushi tofauti upate nyongeza na kushuhudia fainali hii kuona bingwa ni nani msimu huu.

Pia, amesema shindano hilo limekuwa ni daraja la kufunguka kwa fursa nyingi kwani wapo watakaopata ubalozi wa bidhaa kutoka katika makampuni mbalimbali ya biashara.

Kwa upande wake, Meneja Mradi wa shindano hilo, Ombeni Phiri amesema washiriki wamebaki 12 walioingia fainali hivyo, wataendelea kuchuana hadi wiki ijayo mshindi mmoja ataondoka na gari hilo Pia, kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa pili na tatu.

Aidha ameongeza kuwa washiriki hao wakiwa ndani ya jumba hilo walijifunza vitu vingi ikiwemo fursa za kutumia mitandao ya kijamii kujiinua kiuchumi na kukuza majina yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad