Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinyijuma wakati wa mahafali ya 34 ya TaSUBa yaliyofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, alisisitiza kwamba serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia katika taasisi hizo zilizopo chini ya wizara yake.
Alisema taasisi hizo zimekuwa na mchango mkubwa wa kuibua vipaji vya vijana ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasanii na wanamichezo na kujitengenezea ajira kupitia vipaji vyao.
“Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia, itaendelea kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia katika taasisi ya TaSUBa na Chuo Cha Malya, lengo ni kuhakikisha zinafikia malengo ya kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi katika sekta ya sanaa na michezo.
“Matokeo ya uwekezaji huu unaofanywa na serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha tunaimarisha na kuongeza ubora wa mafunzo yanayotolewa na pia kutoa nafasi zaidi kwa vijana wenye vipaji vya sanaa na michezo,” alisema.
Pia Naibu Waziri alisisitiza kwamba ana mpango wa kubalisha sheria na kanuni za vyama na mashirikisho ya sanaa, kuhakikisha kila atayekuwa anataka kugombea nafasi ya uongozi katika soko la sanaa awe amesoma angalau kozi fupi TaSUBa.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya TaSUBa, Dkt. Herbert Makoye alisema jumla ya wanafunzi 270 walihitimu katika fani mbalimbali ambapo astashahada walikuwa 158 na stashahada wahitimu 112.
Alisema wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwapa fedha za maendeleo ambazo zimeiwezesha taasisi hiyo kufanya ukarabati wa baadhi ya majengo na kununua vifaa vya kufundishia.
“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutupatia fedha za maendeleo ambazo zimeiwezesha taasisi kufanya ukarabati wa baadhi ya majengo na kununua vifaa vya kisasa vya kufundishia.
“Tupo katika mchakato wa kuanzisha televisheni na redio yetu kwa ajili ya kupanua wigo wa mafunzo kwa wanafunzi mbalimbali,” alisema Dk. Makoye.
Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA', akimkabidhi cheti staa wa muzuki wa hip hop Farid Kubanda 'Fid Q' baada ya kuhitimu kozi fupi ya Mafunzo ya utawala na Masoko katika sanaa katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), wakati wa mahafali yaliyofanyika mwsihoni mwa wiki katika taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.

No comments:
Post a Comment