HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 5, 2023

KATIBU MKUU UCHUKUZI AIPONGEZA TCAA KWA KUKIBORESHA CHUO CHA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (CATC)

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara ametembelea Banda Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5-8,2023 na kuvutiwa na Mradi mkubwa wa Serikali wa kuboresha Chuo kwa kujenga miundombinu ya CATC ikiwemo majengo mapya yanayoendana na viwango vya Kimataifa.

Prof Kahyarara alipewa maelezo juu ya mradi huo na Mkuu wa Mafunzo ya Uongozaji Ndege CATC Godlove Longole na pia alielezwa kuhusiana kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

Kwa upande wake Prof Kahyarara ameipongeza TCAA kwa usimamizi mzuri wa Chuo na kukitaka chuo kuendelea kujitangaza zaidi ili kisikike na kuwafikia watu wengi Zaidi ndani na nje ya nchi.

CATC ni moja ya vyuo  vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC)  na  ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo  Afrika na 35 duniani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole alipokuwa anaelezea kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara akisoma moja ya kitabu cha CATC alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati wa Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5-8,2023

Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye Banda la Mamlaka hiyo wakati wa  Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad