HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 21, 2023

Halotel yatembelea na kutoa msaada kituo maalum cha Salt Special Centre VTS,msakuzi jijini Dar es Salaam

 

 
Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kupitia huduma yake ya kifedha ya Halopesa, katika kuelekea kipindi cha msimu wa Sikukuu imeamua kusherehekea kwa kutembelea kituo cha kulelea watoto maalum cha Salt Special Centre kilichopo Mbezi Msakuzi,jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam Desemba 20,2023 katika kituo hicho, Ofisa masoko wa Halotel, Roxana Kadio, amesema wana furaha kubwa kusherehekea pamoja na ndugu katika msimu huu adhimu kabisa wa sikukuu kwa kuwatembelea, kuwashika mkono pamoja na kula nao chakula kuwatia moyo ambao wanalea watoto wenye uhitaji maalum.

“Katika kipindi hiki cha Sikukuu tumeona ni vema kuwa karibu na kituo hiki chenye takribani watoto 42 wanaosumbuliwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwa ni pamoja na kupata pamoja chakula cha mchana kwani ni jukumu letu kurudisha shukrani kwa jamii,” amesema Roxan.

Amesema Halopesa pamoja na kutembelea kituo cha Salt Special Centre, imewazawadia vitu mbalimbali kama nguo, chakula, sabuni, kulingana na mahitaji ya kituo husika,wakati huo huo wakapata wasaa wa kujumuika nao pamoja kwa chakula cha mchana, ambapo Halopesa imefanya hivyo kwa kuonesha upendo, thamani na kujali katika jamii kwa ujumla.

Ameongeza kuwa Halopesa inafurahia kujumuika na marafiki na itaendelea kuangalia namna nyingine zaidi ya kuonesha ulimwengu thamani na upendo ikiwa pamoja na kuboresha huduma za kifedha kupitia simu ili ziwe bora kwa ajiri ya wateja wa halotel.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho cha Salt Special Centre, Rebecca Lebi, amesema kuwa ni furaha kubwa mno kupata watu wanaotambua thamani, utu na na kujali utu wa watu wengine kama walivyo fanya Halotel.

“Nina furaha mno kuona kampuni kama Halotel kutambua thamani yetu kisha kuamua kuja kututembelea na kutuletea zawadi mbalimbali katika kipindi hiki cha sikuu, hii itasaidia na sisi kujiona ni sehemu ya jamii kama jamii zingine hivyo tunaomba taasisi nyingine zijitokeze kwa kuchangia mahaitjai mbalimbali katika kituo chetu,” amesema.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad