HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 1, 2023

CHUO KIKUU CHAWAFUNDA KWA SIKU NANE WATUMISHI WA AFYA WA ILALA

 

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Muba Seif, akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya wa wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Novemba 30, 2023, Baadhi ya atumishi wanaotoka katika vituo vya Afya vilivyopo manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa katika mafunzo yaliyoandaliwa na chuo Kikuu Mzumbe.

CHUO Kikuu Mzumbe kuwafunda watumishi wanaotoka katika vituo vya Afya vilivyopo manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam Novemba 30, 2023, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Muba Seif, amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa watumishi wa sekta hiyo ya afya kwa awamu ili kuwapa uelewa wa kutosha juu ya masuala ya fedha, Ugavi, Utawala na uongozi.

Amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa maafisa wa Afya, Madaktari, Wauguzi wanaofanya kazi katika vituo vya afya na hospitali katika wilaya hiyo.

"Kikubwa tulikuwa tunawapa elimu juu ya namna ya kuzifahamu taarifa za fedha na uelewa juu ya namna ya kutumia taarifa hizo kufanya maamuzi sahihi."

Dkt. Muba amesema kuwa ametoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa taarifa za fedha kwa matumizi ya ofisi na matumizi binafsi katika kuendesha maisha kwani kuna maisha baada ya kustaafu.

Dkt. Muba amesema kuwa Mafunzo hayo yanadumisha uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Manispaa ya Ilala.

"Manispaa ya Ilala itaendelea kutuamini na inaweza kutuomba tutoe mafunzo mengine kwenye sekta nyingine zilizo chini ya manispaa ukitoa sekta hii ya Afya ambao wameshapata mafunzo haya." Ameeleza

Kwa Upande wa mwakilishi wa Wataalamu wa afya, Sitishiki Juma amesema kuwa Mafunzo hayo ni ya manufaa makubwa na yatawawezesha kuandaa hesabu za fedha kitaalamu zaidi na hivyo kuimarisha usimamizi na matumizi bora ya rasilimali fedha kwa lengo la kutoa huduma bora kwa jamii.

Akizungumzia kuhusiana na manufaa ya mafunzo hayo Sitishiki amesema kuwa wameyapata kwa muda muafaka kwani serikali inahimiza usimamizi bora warasilimali katika taasisi za serikali.

Dkt. Faisal Issa ambaye atawafunda watumishi wa sekta hiyo ya Afya kutoka Manispaa ya ilala kuhusu uongozi wa matokeo na utawala bora akizungumzia umuhimu wa mafunzo kwa watumishi, alitoa pongezi kwa niaba ya uongozi wa Chuo kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kwa kuona umuhimu wa kujenga uwezo wa watumishi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad