HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 10, 2023

Bilioni 2.1 zapatikana ndani ya Siku Tano-Msajili wa Hazina Mchechu

 

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akipokea Hundi ya Bilioni Mbili kutoka kwa Msajili wa Hazina Nehemiah Mchchu kwa ajili ya Waathirika wa Mafuriko wilayani Hanang Fedha hizo ni mchango wa Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali ,Ikulu Chamwino jijini Dodoma

*Ni kwa ajili ya waathirika mafuriko Hanang

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
OFISI ya Msajili wa Hazina imesema kuwa baada ya kutokea mafuriko ya Katesh wilayani Hanang wameratibu kwa siku tano kwa mashirika na wakala wa serikali na kupatikana sh.Bilioni 2.1 kwa ajili ya kusaidia waathirika mafuriko hayo.

Akizungumza mbele ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu wakati kukabidhi hundi kwa ajili ya waathirika wa Mafuriko Hanang amesema kuwa wakati siku mbele majanga haya yakitokea hawatasubiri bali watakwenda moja kwa moja kusaidia.

Amesema kuwa mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali katika kuonekana ya mchango ni wajibu wake uonekene pale yanapotokea majanga na kuonekana thamani yake kwa watanzania.

Amesema kuwa Mh.Rais amepitia wakati mgumu na kufanya kusitisha ziara yake katika Falme za Kiarabu katika Mkutano wa Mazingira hivyo tumeona kwa hali hiyo tuweze kuchanga japo kidogo kutokana na tatizo lililo mbele yetu.

Mchechu amesema kuwa wakati kuna mabadiliko yanaendelea kufanyika katika mashirika ya umma hali ambayo yatafanya kuonekanaa yakifanya kazi na kuleta tija ya maendeleo

Aidha ameziomba Taasisi zingine kuwiwa kuchangia kwa katika janga hilo katika kutoa faraja kwa wananchi walioathirika na janga la mafuriko wilayani Hanang.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad