HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 6, 2023

BASATA YATOA WITO KWA WASANII KUWASAIDIA WATANZANIA WALIOATHIRIKA NA JANGA LA MAFURIKO WILAYA YA HANANG

SERIKALI na wadau mbalimbali wakiendelea kusaidia wahanga wa maafa yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang Mkoani Manyara Wasanii nchini wameombwa kuungana na kutoa michango yao ili kusaidia familia zilizo athirika.

Wito huo umetolewa na Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kama kuna Msanii yuko tayari kwenda kutoa msaada, Baraza lipo tayari kumsindikiza, au Wasanii wanaweza kuwasilisha michango yao na Baraza la sanaa litawakilisha michango hiyo.

Aidha, Dkt Mapana Ameongeza kuwa wakati nchi inapitia kwenye kipindi cha maombolezo Baraza hilo inatambua kuwa Hanang kulikua na wasanii ambao wao na familia zao wameathirika hivyo linahimiza wasanii kuungana kwa pamoja kwakutoa pole na misaada mbali mbali.

Hata hivyo Mapana ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watanzania wote kuungana na wahanga hao katika kuwafariji katika kipindi hiki kigumu kwa kutoa mahitaji mbalimbali kunusuru Kaya zilizopata athari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad