KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi Beng'i Issa amewakumbusha Wanawake kuwa na desturi ya kuweka akiba na kuwa na nidhamu pamoja na kitumia ujuzi na teknolojia za kisasa katika biashara zao.
Katibu Mtendaji ameyasema hayo katika Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W). Maulid hiyo iliyofanyika jana Novemba 26,2023 katika Msikiti wa Akram uliopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
"Katika kupiga hatua yoyote ya kimaisha lazima uwe na nidhamu hasa kwenu wakina mama wa dini ya kiislam mnaojishughulisha na kuzalisha uchumi wa taifa lazima uwe na nidhamu namna unavyoendesha biashara hiyo kuanzia kutoa huduma kwa wateja wako, kutunza fedha yani kujiwekea akiba ili kuweza fedha na fedha hizo ziweze kujizalisha mara mbili yake."
Pia amezungumzia swala la wazazi kutenga muda na kupata nafasi ya kuzungumza na watoto wao.
"Tuwaandae watoto wetu katika kukabiliana na kila kitu ili tuwatengeneze mazingira ya kuona kila kitu mapema kuliko kusubiri litokee tatizo ndio Wayne ni mapya hivyo wazazi tuweke muda wa kuzungumza na vijana wetu dunia kwa sasa imechafuka hivyo kupitia dini yetu tuweze pia kuendelea kuwalea katika maadili."
Sanjari na hilo Katibu Mtendaji aliendesha harambee ya uchangiaji wa fedha kwa ajili ya msikiti huo wa Akram ambapo aliwasilisha kiasi cha fedha shilingi laki tatu huku akisisitiza zaidi kuwa huo ni mwanzo tu ataendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi huo pamoja na idara ya Wanawake.
Pia ametoa wito kwa Wanawake kuwa na Imani na kuabudu pamoja na kujifunza na kujitoa katika kuzikimbilia fursa za kiuchumi.
"Mwanamke akiwezeshwa anaweza kulikomboa taifa hivyo tuendelee kuzalisha uchumi lakini tusiache kujenga imani na kufanya ibada. "
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake, Masjid Akram, Mwajuma Kingwande amesema wameadhimisha Maulid hiyo ya Mtume Muhamad (S.A.W) ili kuhamasisha Kizazi cha sasa na kijacho kuona umuhimu wa siku hiyo na kufuata Sifa zake, tabia, mwenendo wake kizazi cha sasa.
Amesema Idara ya Wanawake Masjid Akram inajihusisha pia na masuala ya kijamii kama kufutirisha kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa wasio na uwezo pia kutembelea vituo vya Watoto yatima sambamba kutoa misaada ya kijamii bila kujali dini.
Nae Makamu Mwenyekiti wa idara ya Wanawake Masjid Akram ameongeza kuwa shughuli hizo zimekua zikifanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na umoja huo Wakina mama wapatao 30 kwa zaidi ya Miaka 18 huku matarajio makubwa ni kusaidia watu wenye uhitaji ikiwemo watoto yatima pamoja Wanawake wenye Uhitaji Wajane na Mahospitalini.
Makamu Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake Masjid Akram Zainab Asman Katoro akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Beng'i Issa wakati wa Maulid ya Mtume Muhamad (S.A.W) Maulid iliyofanyika Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Beng'i Issa akizungumza na Wanawake wa dini ya kiislam waliohudhuria katika Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyoandaliwa na Idara ya Wanawake Masjid Akram Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
Wanawake wa dini ya Kiislam kutoka vyuo mbalimbali waliohudhuria katika Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyoandaliwa na idara ya Wanawake Masjid Akram Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam
Muimbaji wa Kaswida Arafa akitumbuiza katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyoandaliwa na Idara ya Wanawake Masjid Akram Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment