HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 10, 2023

Wanafunzi 49 Elimu Maalumu Kunufaika na Bweni

 


WANAFUNZI wa shule ya Msingi na ufundi Namtumbo iliyopo wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma Kunufaika na bweni lililojengwa Kwa thamani ya shilingi milioni 100 Kwa ajili ya wanafunzi wa kitengo Cha elimu maalumu Shuleni hapo.

Bibiana Adamu Buyanza mwalimu wa wanafunzi wa elimu maalumu katika shule ya msingi na ufundi Namtumbo alisema kujengwa Kwa bweni Hilo litawasaidia watoto walemavu ambao wengi wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na kutembea umbali mrefu kutoka Majumbani kwao na kufika shuleni

Aidha Bibiana alidai kujengwa Kwa bweni hilo litasaidia kuondoa utoro wa watoto wenye mahitaji maalumu na kuwafanya waweze kukaa shuleni hapo na kuhudhuria masomo Kila siku.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi na ufundi Namtumbo Mustapha Ponera alidai shule yake ilipewa fedha milioni 100 kutoka Lanes II Kwa ajili ya kujenga bweni la watoto wenye mahitaji maalumu Shuleni hapo.

Hata hivyo Ponera alidai ujenzi wa bweni Hilo lipo katika hatua za umaliziaji na mara ujenzi huo utakapo kamilika wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu wataanza kulala katika bweni Hilo.

Kitengo Cha elimu maalumu katika shule ya msingi na ufundi Namtumbo kina jumla ya walimu 4 kukiwa na walimu wa like 2 na wakiume 2 huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni 49 wanafunzi wavulana 33 na wanafunzi wa kike 16 .

Shule ya msingi na ufundi Namtumbo IPO katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo Ina jumla ya wanafunzi 845 ambapo kati ya wanafunzi hao , wanafunzi 49 ni wanafunzi wa kitengo Cha elimu maalumu ambao wamejengewa bweni Hilo waweze kulala shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad