MUASISI wa Kliniki ya 4A9 African Trust, Dk Tr Msigwa ameiomba serikali kuangalia upya sera ya afya kwa watu binafsi wanaotumia tiba mbadala kutibu ugonjwa wa Ukimwi.
Amesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na vikwazo mbalimbali pale wanapoeleza kuwa wanauwezo wa kutibu Ukimwi na kumfanya muathirika kuwa na afya njema.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Dkt Msigwa amesema kuelekea Siku ya Ukimwi duniani, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuweka mazingira bora yanayowasaidia kutoa huduma zao.
Amesema kuwa kama Mtanzania amefanya jitihada kubwa kuondoa mstari mmoja kwa watu wenye Virusi Vya Ukimwi na kubaki na mstari mmoja.
Amesema watu hao wamekuwa wakitumia dawa za kisayansi kwa muda mrefu na kukata tamaa na kwamba walipomtafuta aliwasaidia kurudisha afya zao.
Ameeleza kuwa hayo aliyoyafanya yanachangiwa na mazingira mazuri na rafiki yaliyokiwepo nchini.
"Nitatoa ripoti ya watu 100, 500 na 1,000 ambao wote walitumia tiba zetu na kuondoa mstari mmoja badala ya miwili iliyokuwepo awali. Sibahatishi kwenye magonjwa nyemelezi na kuondoa mstari mmoja," amesema Dkt Msigwa.
Dkt Msigwa amesema ili kukabiliana na ugonjwa huo na kufikia viwango vilivyowekwa duniani, lazima kuhakikisha jamii inajitambua na kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kupima.
"Tunaposema kwamba tunaweza kutibu Ukimwi kwa mtu ambaye anamaambukizi tunakumbana na vikwazo vingi lakini sera ikiangaliwa vizuri, tunaweza kusaidia taifa kufikia lengo tulilokusudia," amesema.
Amesema amekuwa akikutana na vijana wengi hususan wenye umri wa miaka 18 hadi 20 ambao wana maambukizi na kwa wiki hufikia idadi ya watu zaidi ya 200.
"Tatizo zaidi ni kule wanakochukulia dawa lugha na mazingira sio rafiki na ndio maana watu wengi hutafuta njia mbadala kuweza kurekebisha afya zao," amesisitiza.
Aidha, amewataka watanzania kujitambua na kujilinda ili wawalinde wenzao na kukomesha ugonjwa huo ambao unamaliza nguvu kazi ya taifa.
No comments:
Post a Comment