HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 25, 2023

MISA TAN, VIKES WAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUTOKOMEZA UKATILI WA WANAWAKE, KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA NA UHURU WA HABARI


Mkurugenzi wa MISA TAN Elizabeth Riziki akizungumza katika mkutano huo unalenga kuleta pamoja wahusika wa serikali, wataalamu wa vyombo vya habari, na wawakilishi kutoka taasisi za kijamii katika  kuimarisha ushirikiano, kubadilishana mawazo, na kutafuta mikakati itakayochangia kukuza usawa wa kijinsia na uhuru wa vyombo vya habari.

Mjumbe wa  GEMSAT Rose Hajj Mwalimu  akichangia mada katika mkutano wa wadau mbalimbali kuhusiana na kutafuta  mikakati itakayochangia kukuza usawa wa kijinsia katika vyombo vya habari ,jijini  Dar es Salaam. 

Baadhi ya wadau katika mkutano wa kutafuta mikakati itayochangia kukuza usawa wa kijinisia katika vyombo vya habari ,jijini Dar es Salaam.

Wakili James Marenga akitoa mada katika mkutano huo unalenga kuleta pamoja wahusika wa serikali, wataalamu wa vyombo vya habari, na wawakilishi kutoka taasisi za kijamii ili kuimarisha ushirikiano, kubadilishana mawazo, na kutafuta mikakati itakayochangia kukuza usawa wa kijinsia na uhuru wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa GEMSAT Dominica Haule akichangia mada katika mkutano wa wadau mbalimbali kuhusiana na kutafuta  mikakati itakayochangia kukuza usawa wa kijinsia katika vyombo vya habari ,jijini  Dar es Salaam.
Mwenzeshaji wa GEMSAT  Gladness Munuo akiwasilisha mada kuhusiana na masuala ya usawa wa kijinsia katika vyombo vya habari nchini namna ya kupambana na ukatili ndani vyombo hivyo.bikini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake tareheNovemba 25, Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na VIKES wamefanya mkutano wa Kuimarisha Muungano wa Usawa wa Jinsia na Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo wenye kauli mbiu "Kujenga Daraja: Mkutano wa Usawa wa Kijinsia na Uhuru wa Habari", leo Novemba 24,2023 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa MISA TAN Bi. Elizabeth Riziki amesema mkutano huo unalenga kuleta pamoja wahusika wa serikali, wataalamu wa vyombo vya habari, na wawakilishi kutoka taasisi za kijamii ili kuimarisha ushirikiano, kubadilishana mawazo, na kutafuta mikakati itakayochangia kukuza usawa wa kijinsia na uhuru wa vyombo vya habari.

“Malengo ya mkutano huu ni kuunda jukwaa kwa wahusika wa serikali, wataalamu wa vyombo vya habari, na wawakilishi wa taasisi za kijamii kujenga uhusiano, kubadilishana mawazo, na kuchunguza ushirikiano unaowezekana”,amesema.

“Lengo jingine ni Kujiandaa kwa Siku 16 za Uanaharakati kwa kuunganisha nguvu katika kampeni kubwa ya kimataifa ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Dhuluma za Kijinsia, kuunda msukumo kwa juhudi endelevu zaidi baada ya tukio la siku moja”,ameeleza.

Malengo mengine ni kukuza Usawa wa Kijinsia kwa kushirikisha washiriki katika mazungumzo, na mawasilisho yanayobainisha jukumu la vyombo vya habari katika kukuza usawa wa kijinsia na kupambana na dhuluma dhidi ya wanawake. Kuhamasisha maendeleo ya ripoti na hadithi zinazozingatia masuala ya kijinsia.

“Lengo jingine ni Kukuza Uhuru wa Habari kwa Kusisitiza umuhimu wa vyombo vya habari huru na visivyopendelea katika jamii ya kidemokrasia. Kujadili changamoto zinazokabiliwa na wataalamu wa vyombo vya habari na kuchunguza njia za kulinda na kukuza uhuru wa habari”,amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad