Na Mwandishi Wetu, Kisarawe
MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa (JWT), Hamis Livembe, amewataka
wafanyabiashara Tanzania kufanya kazi kwa bidii kwa sababu Rais Samia
Suluhu Hassan ameifungua nchi kiuchumi.
Amesema wana wajibu wa
kujivunia juhudi za Rais Samia katika kushughulikia kero zao na kufungua
milango ya majadiliano jambo ambalo halikuwahi kufanyika miaka ya
nyuma.
Livembe ameyasema hayo leo, wakati akizungumza na
wafanyabishara wilayani Kisarawe mkoani Pwani, katika mwendelezo wa
ziara za viongozi wa JWT kusikiliza kero za wafanyabiashara nchi nzima.
Amesema
awali wafanyabishara walikuwa hawana nafasi ya kusikilizwa isipokuwa
wakati inapotokea migomo na maandamano lakini tangu utawala wa Rais
Samia, wamepewa nafasi ya kujisemea na kusikilizwa.
"Tutembee
kifua mbele, tufanye biashara kwa amani na utulivu, bila kusahau
kutimiza wajibu wetu. Tumekutana hapa leo tujadili matatizo yetu kipi
kinatukwamisha kufanya biashara kwa utulivu ili kwa kushirikiana na
serikali tukae meza moja na tuyamalize," amesema Livembe.
Ametolea
mfano wa moja ya kero ambazo imefanyiwa kazi ni faini ya kutokutoa
risiti kwa mteja au kutoandika jina ambayo awali ilikuwa Sh. milioni 4.5
lakini imeshushwa hadi Sh. 1.5 baada ya wafanyabishara kulalamika.
Naye
Mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya JWT, Ismail Masoud, amesema katika mikoa
12 waliyopita wamesikiliza kero nyingi ambazo sinafanana na tayari
nyingine zimeanza kufanyiwa kazi.
Nao wafanyabiashara wa Wilaya
ya Kisarawe, walilalamikia kodi za kero zinazotozwa na halmashauri na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwamo ya jengo la fremu anayotozwa
mpangaji badala ya mwenye nyumba.
Ziara hiyo inaendea leo katika wilaya za Kibiti na Mkuranga mkoani humo.
Tuesday, November 7, 2023
Livembe: Wafanyabiashara tunajivunia Rais Samia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment