HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 23, 2023

Lameck Ditto aipeleka Mahakamani MultChoice Tanzania

Mwandishi Wetu

Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini, Bw.Lameck Ditto ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iamuru Kampuni ya MultiChoice Tanzania Limited imlipe fidia ya Sh 6 Bilioni mara baada ya Kampuni hiyo kutumia wimbo wa Nchi Yangu aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake.

Lameck Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Benard Bwakeya ameiomba Mahakama iamuru alipwe Milioni 200 kutokana na madhara ya jumla, pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo.

Ditto alitoa ushahidi wake kwa saa 6, mbele ya jaji Hamidu Mwanga wa Mahakamani hiyo katika kesi ya madai, akiilalamikia MultiChoice Tanzania Limited kutumia wimbo huo kwenye matangazo yao ya biashara kipindi cha Kampeni ya Afcon 2019.

Akiwasilisha ushahidi wake, alidai, MultiChoice imempora fursa ya kunufaika na kazi yake kupitia wimbo huo.

Miongoni mwa vielelezo alivyoviwasilisha Mahakamani hapo ni mawasiliano ya barua pepe (email) ambayo alidai alifowadiwa na Emmilian Mallya aliyekuwa mratibu wa Tamasha la Urithi ambayo ilionyesha ushiriki wa wimbo wake huo kwenye Tamasha hilo.

"Mheshimiwa jaji, huu ni wimbo wangu na mimi ndiye mmiliki, niliutunga wa kwanza nikaimba mwenyewe, nikaombwa nitunge wa pili kwa ajili la Urithi ambao umeimbwa na wengi," alidai Ditto wakati akitoa ushahidi wake.

Awali, Wakili anayeiwakilisha MultiChoice alidai walitumia Wimbo wa Nchi Yangu, lakini sio huo unaolalamikiwa na mdai.

Hata hivyo, Jaji Hamidu alisema, kinacholalamikiwa Mahakamani hapo ni Wimbo wa Nchi Yangu uliotumiwa na kampuni hiyo, sio wimbo wa Nchi yangu mwingine.

Katika ushahidi wake, Ditto pia aliwasilisha flash Disc yenye audio na video za matangazo anayolalamikia na nyimbo hiyo ambayo alidai yeye ndiye mmiliki halali.

Kabla ya Mahakama hiyo kupokea kielelezo hicho, wakili anayeiwakilisha Multi Choice Tanzania Limited, Mlano Mlekano alihoji uhalali wa video hizo kama si za kutengenezwa.

Kwenye ushahidi wake, Ditto alidai ni halali na endapo links za matangazo hayo hazijafutwa, Mahakama iridhie waangalie kwenye google, na Jaji Mwanga aliliridhia ombi hilo, na video hiyo ilipochezwa, ikafunguka na kumuonyesha mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Akida Mapunda akihamasisha Afcon huku kukiwa na matangazo ya DSTV na katika (background) ulisikika wimbo wa Nchi Yangu.

Ditto pia aliwasilisha vielelezo vingine ambavyo Mahakama ilivipokea kama ushahidi wake.

Nje ya Mahakama, wakili wa Ditto, Elizabeth Mlemeta alisema kesi hiyo imeanza kusikilizwa na upande wa mdai una mashahidi watano.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad