HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 10, 2023

Katibu Mkuu UVCCM Aeleza CCM Walivyojipanga Kuelekea Uchaguzi 2024, Adai Hawatokuwa na Huruma

 


Njombe

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndugu.Faki Lulandala amesema wao Chama cha Mapinduzi kwa sasa akili zao ni uchaguzi na wamejiandaa kushinda katika chaguzi zote ikiwemo serikali za mitaa hapo mwakani 2024 pamoja na uchaguzi mkuu wa 2025 bila kuonea huruma Chama chochote.

Lulandala ameeleza hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa Chama hicho katika ziara yake ya kawaida ndani ya mkoa huo ambako ndio nyumbani kwake iliyokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi na wanachama wa mkoa wa Njombe kwa kumuunga mkono kwenye shughuli zake za siasa ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais Dkt.Samia kuwa katibu mkuu wa UVCCM.

"Uchaguzi wa mwakani ni mkubwa kwasababu ndio unaotoa picha nini kitatokea 2025 kwa hiyo tunawapiga vizuri 2024 na kwa kweli akili zetu zote sasa hivi tunafikiria uchaguzi,tumejiandaa kushinda na tutashinda wala hilo halina mjadala kwasababu serikali ya Rais Samia imetekeleza vizuri Ilani ya Chama cha Mapinduzi"amesema Lulandala

Aidha amesema Chama hicho hakitaweza kuona huruma kwasababu linapokuja swala la maendeleo watu wote wanajua nani wa kuleta maendeleo linapokuja swala la nani asimamie maendeleo na hawahitaji kujaribisha kwasababu wanajua sumu haionjwi.

"Na hatuna huruma sisi tupo tayari kushinda mitaa yote na vijiji vyote,haya mambo ya kusema aaa sasa kidogo na upinzani unatakiwa uwepo ni kweli lakini ninyi mkipata tu nafasi mmekwenda Canada sijui Ubeligiji mkirudi mnaaza kusema boda boda sio kazi"ameongeza kusema Lulandala

Licha ya kuzungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Lulandala amefanikiwa kuzungumza na vikundi mbali mbali ikiwemo maafisa usafirishaji kwa njia ya Piki piki wa mjini Njombe,kikundi cha vijana Wilayani Wanging'ombe pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule shikizi ya sekondari Igwachanya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad