HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 15, 2023

HaloPesa Yazindua 'OKOTA NA HALOPESA'

 

 Kuelekea Katika Msimu wa Sikuukuu Halotel ikiwa kampuni inayosifika nchini kupitia huduma yake ya kifedha ya HaloPesa, imekuja kivingine na promosheni kabambe ya OKOTA NA HALOPESA leo.


Wakiwa kampuni inayokua kwa kasi sana HaloPesa, imeendelea kutoa huduma bora za HaloPesa kwa gharama nafuu kote mijini na vijijini.

Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi za Halotel Tanzania, Afisa masoko Roxana Kadio alisema “Tunafuraha kubwa kuwaletea wateja wetu promisheni hii kabambe ya Okota na HaloPesa, inayowapa wateja wetu fursa ya kujishindia Fedha Taslimu hadi Tsh Millioni Moja, kila wanapotumia HaloPesa Lipa Hapa kupitia *150*88# au kufanya miamala mbalimbali kama kutuma pesa kwenda HaloPesa, kutuma pesa kwenda mitandao mengine, kutuma pesa kwenda benki, kulipia billi, Lipa hapa nakadhilika kupitia HaloPesa App. Zaidi ya wateja 3.5m wanaendela kufurahia huduma zenye ubora na kwa gharama nafuu muda wowote.

Kampeni ya Okota na HaloPesa imelenga kuwazawaidia wateja wetu katika msimu huu wa sikukuu kila wanapofanya miamala ya Lipa Hapa kupitia USSD na miamala mengine ya HaloPesa kupitia HaloPesa App itakayomuwezesha kuingia katika droo ya kila siku, wiki na mwezi. Aliongezea Roxana.

Kampeni ya Okota na HaloPesa ni kwa ajili ya wateja wa HaloPesa ambayo itakuwepo kwa miezi mitatu (3) na jumla ya wateja 300 watakuwa washindi. Kila mteja wa HaloPesa anaalikwa kushiriki kwenye promosheni hii, hivyo tunawahamashisha wateja wetu kufanya miamala mingi ili waweze kupata nafasi kubwa ya kushinda.

HaloPesa inafurahia kuzindua promosheni hii leo na itaendelea kufikiria njia nyingine Zaidi za kufanya ulimwengu wa huduma za kifedha kupitia simu kuwa bora Zaidi kwa ajili ya wateja wetu.
Afisa Masoko Halopesa Roxana Kadio (kulia) akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya wateja yenye jina la “Okota na Halopesa” uliofanyika jijini Dar es salaam. Promosheni hii ni maalum tunapoelekea Msimu wa Sikukuu za mwisho wa Mwaka. Promosheni hii kabambe ya Okota na HaloPesa, inawapa wateja wetu fursa ya kujishindia Fedha Taslimu hadi Tsh 1,000,000, kila wanapotumia HaloPesa Lipa Hapa kupitia *150*88# au kufanya miamala mbalimbali kama kutuma pesa kwenda HaloPesa, kutuma pesa kwenda mitandao mengine, kutuma pesa kwenda benki, kulipia billi, Lipa hapa nakadhilika kupitia HaloPesa App. Pamoja naye ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Halopesa Joseph Jackson.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Halopesa (kulia) akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya wateja yenye jina la “Okota na Halopesa” uliofanyika jijini Dar es salaam. Promosheni hii ni maalum tunapoelekea Msimu wa Sikukuu za mwisho wa Mwaka. Promosheni hii kabambe ya Okota na HaloPesa, inawapa wateja wetu fursa ya kujishindia Fedha Taslimu hadi Tsh 1,000,000, kila wanapotumia HaloPesa Lipa Hapa kupitia *150*88# au kufanya miamala mbalimbali kama kutuma pesa kwenda HaloPesa, kutuma pesa kwenda mitandao mengine, kutuma pesa kwenda benki, kulipia billi, Lipa hapa nakadhilika kupitia HaloPesa App. Pamoja naye ni Afisa Masoko Halopesa Roxana Kadio.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad