HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 23, 2023

CMSA YAITAKA JAMII KUJIHADHARI NA UPATU HARAMU

 Na Mwandishi wetu, Arusha.


MAMLAKA ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) imeitaka jamii kujihadhari na upatu haramu kwani ni hatari kwa maendeleo na Taifa kwa ujumla.

Meneja uhusiano wa CMSA, Charles Shirima, ameyasema hayo jijini Arusha kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa.

Shirima amesema jamii ijihadhari na matapeli wanaoahidi watu kuvuna pesa nyingi kirahisi hivyo waepuke kupoteza pesa ya jasho lao kupitia upatu haramu.

"Kutokana na hali hiyo Watanzania wanapaswa kujiunga kwenye masoko ya mitaji kwani ni sehemu ya mfumo wa sekta ya fedha unaowezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo ya muda mrefu yaani mwaka mmoja," amesema

Amesema fedha za maendeleo hupatikana kwa kuuza hisa za kampuni, hatifungani na vipande katika uwekezaji wa pamoja.

Mchambuzi fedha mwandamizi wa CMSA, Witness Gowelle, amesema kupitia maadhimisho hayo wametoa elimu kwa wajasiriamali mbalimbali ili kuwajengea uwezo zaidi.

"Elimu mbalimbali tuliyotoa kwa wajasiriamali watanufaika nao kupitia masoko ya mitaji ili kujiepusha na upatu haramu," amesema Gowelle.

Mjasiriamali kutoka wilayani Ngorongoro, Sas Kotete, amesema wengi wameathirika kupitia upatu haramu hivyo elimu waliyoipata kutoka CMSA itawasaidia kuepuka hayo.

Mjasiriamali mwingine wa mkoani Arusha, Naini Losusu ameipongeza CMSA kwa kuwapa elimu hiyo kwani inawajengea uwezo zaidi juu ya upatu haramu

Maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa kupitia kauli mbiu ya elimu ya fedha, msingi wa maendeleo ya uchumi, yanafanyika jijini Arusha, kwa siku sita kuanzia Novemba 20 hadi 26 mwaka huu.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kufungua rasmi maadhimisho hayo Novemba 22, jijini Arusha



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad