HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 16, 2023

Benki ya CRDB yashiriki katika Mkutano wa Pili wa Kisanyansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto

 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (wapili kulia) akizungumza wakati akiongoza ongoza chini ya Taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), kikao maalum cha kujadili namna sekta binafsi na mashirika yanavyotoa mchango wao kwa sekta ya Afya nchini, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Pili wa Kisanyansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto wenye lengo la kuwaleta pamoja wadau muhimu ili kujifunza. Mkutano huo hutumika kama jukwaa kubwa kwa wataalamu wa afya, watunga sera na wadau kukutana ili kushirikiana maarifa, kutathmini athari za mikakati iliyopo, kushughulikia masuala magumu, kufikiria suluhisho za ubunifu, na hatimaye kuleta mabadiliko chanya, unofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es salaam. Wengine pichani ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Grace Maghembe (kulia), Meneja wa Program Kanda ya Afrika Mashariki Agakhan Foundation (wapili kushoto), David Siso pamoja na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile. Picha zote na Othman Michuzi.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, akizungumza katika kikao maalum cha kujadili namna sekta binafsi na mashirika yanavyotoa mchango wao kwa sekta ya Afya nchini, kilichoongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) chini ya Taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Pili wa Kisanyansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto , ndani ukumbi wa Ruaha, Uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es salaam. Katika mkutano huo Bruce Mwile alielezea kuwa Benki ya CRDB mpaka sasa imetoa kiasi cha Bilioni TZS.64.9 kwenye sekta ya afya zilizosaidia ukamilishaji miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya na ununuzi wa vifaa tiba. Benki ya CRDB kupitia sera yake ya uwekezaji kwenye jamii imekuwa ikitenga 1% ya faidia inayopatikana kwenye uendeshaji ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya afya kwa kusaidia kwenye ujenzi wa vituo vya afya, kutoa vifaa tiba kwenye hospitali mbalimbali hapa nchini. Pamoja na hayo imekuwa na mipango endelevu kwa kushirikiana  na tasisi kama JKCI, CCBRT, ORCI na Maisha Bora Foundation ambazo zinasaidia watoto wenye mahitaji ya upasuaji wa moyo, wagonjwa wa saratani na afya ya mama na mtoto. Wengine pichani ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Grace Maghembe (wapili kulia), pamoja na  David Siso, Meneja wa Program Kanda ya Afrika Mashariki Agakhan Foundation (wapili kushoto).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, wakati akizungumza katika kikao maalum cha kujadili namna sekta binafsi na mashirika yanavyotoa mchango wao kwa sekta ya Afya nchini, alichokiongoza chini ya Taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Pili wa Kisanyansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, ndani ukumbi wa Ruaha, Uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es salaam. Katikati ni David Siso, Meneja wa Program Kanda ya Afrika Mashariki Agakhan Foundation.

Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, akisisitiza jambo wakati akizungumza katika kikao maalum cha kujadili namna sekta binafsi na mashirika yanavyotoa mchango wao kwa sekta ya Afya nchini, kilichoongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) chini ya Taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Pili wa Kisanyansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto , ndani ukumbi wa Ruaha, Uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es salaam.


Sehemu ya wadau walioshiriki katika kikao maalum cha kujadili namna sekta binafsi na mashirika yanavyotoa mchango wao kwa sekta ya Afya nchini, kilichoongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) chini ya Taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Pili wa Kisanyansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto , ndani ukumbi wa Ruaha, Uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad