SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazo taarifa za kupotea kwa Watanzania wawili nchini Israel ambao ni miongoni mwa vijana 260 waliopo nchini humo kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa.
Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali nchini Israel inaendelea na juhudi za kuwapata vijana hao ili kuwaleta katika mazingira salama. Familia za vijana hao zimejulishwa kuhusu jitihada hizo na Serikali inaendelea kuwasiliana nao.
Watanzania 9 wanaoishi nchini Israel waliitikia wito wa mpango wa Serikali wa kuwarejesha nyumbani na walipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tarehe 18 Oktoba 2023.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
No comments:
Post a Comment