Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana Tanzania (TYC) Lenin Kazoba, akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 30,2023 jjjini Dar es Salaam wakati wa mjadala wa vijana kuhusu ushiriki wao kwenye michakato ya uchaguzi. Mjadala huo umeandliwa na Taasisi ya Vijana ya Tanzania ( TYC).
Mwalimu wa Msauala ya demokrasia na diplomasia nchini, Deus Kibamba akizungumza na vijana leo Septemba 30,2023 jjjini Dar es Salaam wakati wa mjadala wa vijana kuhusu ushiriki wao kwenye michakato ya uchaguzi. Mjadala huo umeandliwa na Taasisi ya Vijana ya Tanzania ( TYC).
Na Karama Kenyunko Michuzi TV.
KUFUATIA muamko mdogo wa wananchi kupiga kura kipindi cha uchaguzi, Vijana nchini wamependekeza mambo mbali mbali kwa Tume Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ikiwamo kufanyiwa mabadiriko kwa mfumo wa ujiandikishaji kwa wapigakura
Wamesema kama maboresho yatafanyika basi ni wazi itarahisisha ushiriki wa watu wengi hususani vijana ambao mara nyingi wamekuwa wakikosa muamko wa ujiandikishaji na hata kupiga kura.
Mapendekezo hayo yametolewa leo Septemba 30, 2023 jijini Dar es Salaam, wakati wa mjadala wa vijana na ushiriki wao kwenye michakato ya uchaguzi ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana Tanzania (TYC).
Mapendekezo hayo yametolewa jijini Dar es Salaam leo, Septemba 30, 2023 na vijana mbalimbali walipozungumza katika mjadala kuhusu ushiriki wao kwenye michakato ya uchaguzi ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana Tanzania (TYC).
Akizungumza juu ya mapendekezo hayo, Mwalimu wa masuala ya demokrasia na diplomasia, Deus Kibamba amesema kuna haja ya kurahisishwa kwa mifumo hiyo kwani mfumo unaotumika sasa ni wa kizamani na vijana wengi wanajikuta wakishindwa kukaa foleni na kujiandikisha kwa kuwa wana mambo mengi.
Amesema kama mfumo utabadirika na kuwa wa kidigitali utamuwezesha kijana kujiandikisha mwenyewe kwa kutumia simu yake, badala ya kulazimika kwenda kupanga foleni ya kusubiri kuandikishwa.
"Vijana wana mambo mengi kwa hiyo suala la kupanga folani kusubiri aandikishwe ni jambo gumu kwake, tutengeneze mfumo wa kidigitali," amesema
Aidha Kibamba amewataka NEC kuandaa programu tumizi itakayowezesha mfumo huo kufanya kazi ingawa wapo ambao hawataweza kujiandikisha wenyewe hivyo amependekeza kuwepo kwa mawakala watakaoshughulikia kuwaandikisha watu kama unavyofanya mitandao ya simu kwa watu wanaojisajili laini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TYC, Lenin Kazoba amesema majadala huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa 'Kijana Nahodha' unaowalenga vijana 45,000 kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Mradi huu unalenga kuwafikia vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 25 ambao wako mashuleni na wale walioko mtaani ambapo pamoja na mambo mbali mbali wanapewa elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo elimu ya ufundi stadi, afya ya akili na kushiriki michakato ya uchaguzi.
"Mradi huu utatekelezwa kwa miaka sita na unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID)," amesema.
Naye, Raymond Kanegene Mwanasheria, Ofisa Uchechemuzi Mwandamizi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), amesema elimu ni moja ya kikwazo cha vijana katika uchaguzi na kwamba elimu iliyopo ya uraia haitoshelezi kuwashawishi vijana kwenda kushiriki katika michakato ya uchaguzi.
"Elimu iliyopo si rafiki kwa vijana, na mara nyingi inayotolewa huwa na taswira ya matabaka ama ya wazee au wagombea pekee na hata ile elimu tunayopewa darasani kwanza imekaa kwa ajili ya mitihani na haimjengi kijana kuwa raia bora anabaki kusoma kwa ajili ya kujibia mtihani.
No comments:
Post a Comment