HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 1, 2023

UBIA WA TWIGA WAONESHA ATHARI CHANYA ZA KIMAGEUZI ZA UCHIMBAJI MADINI NCHINI, YASEMA BARRICK

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akizungumza na waandishi wa habari katika Mgodi wa North Mara juzi kuhusu athari chanya za ubia wa kimageuzi katika uchimbaji madini kwa kushirikiana na Serikali kupitia kampuni ya Twiga. Kushoto ni Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido.
Mkuu wa Wilaya, Tarime, Michael Mtenjele, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Mgodi wa North Mara kuhusu mipango ya kuimarisha ulinzi na usalama katika Mgodi wa North Mara baada ya kukutana na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow.
Mbunge wa Tarime vijijini, Mwita Waitara akiongea katika mkutano huu.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akimkabidhi ufunguo wa gari Mkuu wa Wilaya Mara, Michael Mtenjele (kulia) lililotolewa na Barrick kwa ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za CSR za mgodi wa North Mara katika Halmashauri ya Wilaya hiyo wakati wa hafla hiyo.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow, akizindua Kamati mpya ya Maendeleo ya Jamii (CDC) ya Halmashaurin ya wilaya ya Tarime ambayo kwa sasa Mwenyekiti wake mpya ni Diwani wa Kata ya Matongo, Godfrey Kigoye.
Viongozi wa mila kutoka koo zote za kabila la Wakurya wakimpatia Rais na CEO wa Barrick, Mark Bristow, zawadi ya beberu la mbuzi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo ya wananchi wa Tarime.
---
Kampuni ya Dhahabu ya Barrick na serikali ya Tanzania zimedhihirisha jinsi uchimbaji madini unavyoweza kuwa na manufaa makubwa pale wachimbaji madini na serikali wenyeji wanaposhirikiana katika kuleta thamani endelevu kwa wadau wote, anasema Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Mark Bristow.

Akizungumza na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki , Bristow alisema ubia ulioanzishwa na Barrick na Serikali uliyoiunda Kampuni ya Twiga ambamo pande zote mbili zinagawana kwa usawa faida za kiuchumi zinazotokana na migodi ya North Mara na Bulyanhulu, unapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa ni ubia wenye mafanikio makubwa, hasa katika nchi zinazoendelea. Aidha, si tu kwamba Barrick sasa ndiyo mchangiaji mkubwa zaidi katika uchumi wa Tanzania kupitia kodi, mishahara, gawio, malipo kwa wasambazaji wa ndani, na uwekezaji katika miradi ya jamii, bali pia kampuni hiyo imethibitisha kwa makampuni mengine ya kimataifa ya madini kuwa nchini humu kunawekezeka.

Tangu mwaka 2019 ilipoichukua migodi hiyo miwili iliyokuwa imekufa, Barrick imeibadilisha na kuifanya kuwa ya kiwango cha kimataifa na hivyo, kutoa mchango mkubwa katika faida halisi ya kampuni. Aidha, katika kipindi hicho, kampuni hiyo imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika uchumi wa Tanzania, huku mwaka huu Twiga ikitambuliwa kuwa mlipaji mkubwa wa gawio kuliko makampuni yote ambayo serikali ina maslahi nayo. Migodi ya Barrick hutumia asilimia 84 ya bajeti yake ya manunuzi kwa makampuni ya ndani huku asilimia 96 ya nguvukazi yao ikiwa ni wananchi wa Tanzania.

Kwa moyo huo huo wa ushirikiano, Barrick imetoa dola milioni 40 kwenye mpango wa ujenzi wa barabara na dola milioni 30 zaidi katika uboreshaji wa suhula za elimu ya juu nchini.Migodi yote miwili iko katika mwelekeo mzuri wa kuufikia mwongozo wake wa uzalishaji wa mwaka 2023 na utafutaji wa madini pia. Kwa sasa, utafutaji madini katika maeneo yote ya Barrick yaliyopewa leseni umeonesha fursa mpya za maendeleo katika maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa mgodi mpya wa chini ya ardhi huko North Mara.

“Ubia wetu wa Twiga si tu kwamba unaongeza thamani katika uchumi wa Tanzania bali pia katika ubora wa maisha ya jamii zinazoizunguka migodi yetu na ambayo iaendelea kustawi. Kuendelea kwetu kujihusisha na jamii hizi na viongozi wao wa vijiji, AZISE za maeneo hayo pamoja na mashirika ya haki za binadamu kunaonesha falsafa ya Barrick ya ubia na dhamira yetu ya dhati ya kuzingatia haki za binadamu katika maeneo tunayofanyia kazi,” alisema Bristow.

Bristow pia alikabidhi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) gari aina ya Toyota Land Cruiser lililotolewa na Barrick kwa ajili ya ufuatiliaji wa miradi ya kijamii inayotekelezwa kutokana na fedha za katika Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zinazotolewa na Mgodi wa Barrick North Mara. Mgodi wa North Mara kwa sasa unatekeleza miradi zaidi ya 100 ya CSR mkoani Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, alisema gari hilo ni muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya CSR kutoka Barrick unaenda vizuri.

Tunashukuru Barrick kwa gari hili, litasaidia wataalamu wetu kufika kwenye miradi kwa wakati na miradi kutekelezeka kwa wakati, ili iweze kunufaisha wananchi wetu,” alisema Kanali Mntenjele.

Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara umetumia zaidi ya shilingi bilioni saba kugharimia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijami kupitia mpango huo wa CSR katika vijiji vyote 88 vya halmashauri ya Wilaya ya Tarime, ambapo asilimia 70 ya kiasi hicho cha fedha kikienda kwenye vijiji vinavyouzunguka.

Katika hafla hiyo, viongozi wa mila kutoka koo zote za kabila la Wakurya walimpatia Rais na CEO wa Barrick, Bristow, zawadi ya beberu la mbuzi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo ya wananchi wa Tarime.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad