HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 4, 2023

Serikali Itahakikisha Kila Mwananchi Anapata Huduma ya Afya ya Msingi Bila Kujali Hali Yake

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati akiufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Oktoba 3, 2023 jijini     Dar es Salaam.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua mkutano huo, unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Oktoba 3, 2023 jijini     Dar es Salaam.na (kushoto kwake) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. John Jungu.
WASHIRIKI wa Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia na kuufungua mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Oktoba 3, 2023 jijini     Dar es Salaam. akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Afisa Masoko wa Hospitali ya Aga Khan Tanzania Rukhsar Kanji , wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi mbalimbali za Afya Tanzania, kabla ya kuufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) uliofanyika Oktoba 3, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu na Viongozi wengine wa Wizara ya Afya alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere  kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania.(Tanzania Health Summit) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hasan, uliofanyika Oktoba 3, 2023 jijini     Dar es Salaam.
(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ally Hassan Mwinyi amesema serikali itahakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma ya afya ya msingi bila kujali hali yake ya kifedha.

Amesema ili kufikia lengo hilo, lazima walenge kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, kuthibiti na kuhakikisha ubora wa huduma hizo katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Akifungua mkutano wa 10 wa Afya Tanzania, Oktoba 4,2023 jijini Dar es Salaam, Dk Mwinyi amesema hiyo ni hatua muhimu katika kuhakikisha jamii yenye afya bora, ambayo inaweza kuchangia maendeleo ya uchumi na ustawi wa taifa.

"Tunatambua mifumo thabiti ya afya ni muhimu kwa ustawi wa wananchi wetu na ustawi wa Taifa kwa ujumla hivyo malengo ya mkutano huu yanalingana na ahadi yetu ya kutoa huduma bora za afya kwa watanzania wote.

Huduma ya afya kwa wote ni muhimu kufikia lengo la kuboresha huduma za afya kwa kila mtanzania," amesema Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi amesema serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya afya kwa kuweka vifaa katika vituo vya afya na zahanati na kuongeza rasilimali watu katika sekta hiyo.

Pia amesema katika bajeti ya maendeleo ya serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 imetenga Sh bilioni 203.4 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa vifaa tiba.

Amesema Sh bilioni 86.5 ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa hospitali za Wilaya, vituo vya afya na zahanati na Sh bilioni 116.9 ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Ameeleza kuwa katika fedha hizo wanategemea kujenga hospitali za halmashauri 45, ukarabati wa hospitali kongwe 31, ujenzi wa vituo vya afya 24 na ukamilishaji wa maboma ya zahanati 376.

"Hii itafanya idadi ya vituo vya afya nchini kufikia 6,953 na kufanya maeneo ya vijijini kufikiwa na huduma za afya ya msingi. Tunaweka mkazo mkubwa katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa afya bora, matumizi sahihi ya huduma za afya," amesisitiza.

Hata hivyo, Rais Mwinyi aliwaomba watoa huduma wote ikiwemo sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kushirikiana nao katika safari hiyo ya kufikia afya kwa wote.

Waziri wa afya Ummy Mwalimu, ameelezea namna ambavyo serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa yanayotokea katika sekta ya afya ikiwa ni kipaumbele, mwelekeo wa sekta ya afya Tanzania bara na malengo ya uboreshaji namna ya kushughulikia magonjwa ya mlipuko.

Kwa Upande wa wa maendeleo katika sekta ya afya wameelezea umuhimu wa uwekezaji katika afya ya msingi kuwa njia pekee itakayoifikisha Tanzania kuwa taifa linalotoa huduma bora ya afya kwa watu wote.

Katika mkutano huo wa kumi wa THS, Rais Mwinyi pia amezindua bodi mpya ya usimamizi ya THS na kukabidhi tuzo kwa baadhi ya taasisi, wadau wa afya kwa kutambua michango yao katika sekta hiyo.

Mkutano huo wa siku tatu ukiwa ni wa kumi ambapo wa kwanza ulifanyika mwaka 2014, unahudhuriwa na watu takribani 900, mada mbalimbali kuhusu masuala ya afya zitawasilishwa sambamba na tafiti 230 ambapo kwa mwaka huu Zanzibar imewasilisha tafiti za kisayansi nyingi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad