Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) kimetoa mafunzo ya ndege nyuki (Drone) kwa jumla ya wahitimu 202 ndani ya kipindi cha miaka mitatu tangu kuanza kutolewa mafunzo hayo hapa nchini yanayotolewa na chuo hicho.
Akiwasilisha mada katika mkutano mkuu wa waandishi wa Habari wa Dar es Salaam (DCPC) Mkuu wa chuo hicho Aristid Kanje amesema mafunzo hayo yalianza kutolewa nchini na chuo hicho mnamo mwaka 2021 kwa ushiriano na wataalam kutoka nchini Afrika Kusini na kuongeza kuwa ndani ya kipindi ya miaka miwili chuo hicho kimefanikiwa kuzalisha wakufunzi wake na sasa mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi wa kitanzania.
Kanje amesema chuo cha CATC ni chuo kinachotambulika kimataifa chenye ithibati kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) na ni miongoni mwa vyuo tisa barani Afrika vinavyotoa mafunzo ya usalama wa anga na ni cha 35 duniani.
Amesema baada ya kuendelea kutoa mafunzo ya ndege nyuki (Drone) sasa wataanza kutoa mafunzo ya Ndege nyuki(Drone) ya masuala ya kilimo
Mkuu wa Chuo hicho cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari amesema Mamlaka hiyo inatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na ndani ya kipindi vya miongo miwili sekte hiyo imeendelea kukua na kuimarika.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akiwasilisha mada katika mkutano mkuu wa waandishi wa Habari wa Dar es Salaam (DCPC) kuhusu kazi zinazofanywa na chuo hicho pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (kushoto) akimkabidhi cheti Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje cha udhamini wa mkutano mkuu wa Waandishi wa Habari wa Dar es Salaam( DCPC)
No comments:
Post a Comment