HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 9, 2023

Benki Ya UBA Yahitimisha Wiki Ya Huduma Kwa Wateja Kwa Kuwashukuru Na Kuwapongeza Wateja Na Watoa Huduma Wake.

 

Dar es Salaam 8 Oktoba 2023: Benki ya UBA imehitimisha ‘Wiki Ya Huduma Kwa Wateja’ kwa kuwapongeza wateja wake pamoja na watoa huduma wa benki kwenye hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo yaliyopo Barabara ya Nyerere jijini.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania, Gbenga Makinde alisema, ‘Nipende kutumia nafasi hii ya Wiki ya Huduma ya Huduma kwa Wateja kuwapongeza na kuwashukuru wateja wetu wote pamoja na wafanyakazi wetu ambao wametufikisha kwenye mafanikio haya makubwa tuliyofikia’.

Nawpongeaza wafanyakazi wote kwa kujitolea kutoa huduma iliyo bora kabisa kwa wateka wetu na hii imekuwa ni nguzo kwenye mafanikio haya tuliyoyapata na kuyasherehekea kwa siku ya leo, bila nguvu ya umoja, kujitolea pamoja na kufanyia kazi kwa pamoja leo hii tusingefikia mafanikio haya tunayosherehekea leo hii katika Wiki ya Huduma kwa Wateja’, alisema Makinde.

Kwa Upande wake Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki hiyo, Flavia Kiyanga ameungana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, kwa kuwapongeza na kuwashukuru wateja na watoa huduma wa benki hiyo na kuongeza kwa kwa kusema, ‘Pamoja na shukrani hizo kwa wateja na watoa huduma wetu nipende pia kusema sasa hivi benki yetu imejitanua zaidi na sasa hivi tupo karibia mikoa yote kwasababu ya mawakala wa kibenki.

“Tuna mawakala zaidi ya mia saba Tanzania nzima kwahiyo hata wakazi wa vijijini nao wanaweza kupata huduma zetu bila wasiwasi wowote na wasiotumia huduma zetu tunaomba waanze kufanya hivyo sasa.
“Pamoja na mawakala hao pia tumefungua matawi kwa wingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Arusha, Mwanza na mikoa mingineyo.

“Kwahiyo huduma zetu zinakua hivyo kupitia wiki hii ya Huduma kwa Wateja tunawaomba wateja wetu wazidi kutuamini na tunawaahidi kutoa huduma bora siku zote”. Alimaliza kusema Flavia Kiyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya UBA Tanzania Gbenga Makinde (kulia) akibadilishana kinywaji na mteja wa benki hiyo Amour Mohammed (katikati) kama ishara ya kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. UBA Tanzania imedhamiria kuendelea kutoa huduma bunifu za kidigitali ili kuongeza huduma bora kwa wateja. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa wa benki hiyo Dora Kyungu.Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya UBA Tanzania Gbenga Makinde (katikati) na Afisa Mwendeshaji wa benki hiyo Flavia Kiyanga (kulia) pamoja na mteja wa benki hiyo Amour Mohammed (kushoto) wakikata keki kama ishara ya kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. UBA Tanzania imedhamiria kuendelea kutoa huduma bunifu za kidigitali ili kuongeza huduma bora kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad