Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeeleza kuwa ina jukumu la kutoa elimu kwa umma kuhusu fursa na faida zinazopatikana katika masoko ya mitaji na kujenga uwezo wa wataalamu wanaotoa huduma katika kada hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, CPA Nicodemus Mkama, akizunguma katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la masoko ya mitaji kutoka vyuo vikuu jijini Dar es Salaam, amesema utoaji wa elimu ya fedha kwa umma na kujenga uwezo wa wataalam wanaokidhi viwango vya kimataifa ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha,(Financial Sector Development Master Plan 2019/20 – 2029/30.
Amesema mpango huo wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu.
Mkama amesema CMSA, iliendesha Shindano kwa Wanafunzi wa Vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu, kuhusu uelewa, ueledi wa masoko ya mitaji na uwekezaji wa pamoja kwa kutumia njia ya mitandao ya kielektroniki yaani simu za mikononi na intaneti.
Amesema shindano hilo limeweza kuvutia Mamlaka za Masoko ya Mitaji za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kuja nchini kujifunza jinsi ya kuendesha mashindano kama haya katika nchi zao kwa kutumia simu za mkononi na intaneti.
Aidha amesema mamlaka hiyo imeweka mpango wa kuwawezesha washiriki wa shindano kuwa wawekezaji halisi.
Katik jitihada za kuongeza idadi, ueledi na ufanisi wa wataalamu wa masoko ya mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa wenye lengo la kukuza na kuendeleza masoko ya mitaji hapa nchini, Mamlaka inashirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Uwekezaji na Dhamana (CISI) ya nchini Uingereza, kuendesha mafunzo yanayotambulika kimataifa,”amesema.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo yanajenga uwezo na ufanisi kwa watendaji wa masoko ya mitaji pamoja na ujuzi kwa wahitimu unaowawezesha kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ya sekta ya masoko ya mitaji na dhamana ulimwenguni.
Picha ya pamoja baina ya Viongozi na washikiri wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa CMSA,sekta za fedha na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa shidano la Taasisi za elimu ya juu na vyeti kwa wahitimu wa kozi za watendaji katika masoko ya mitaji.
.Afisa Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) ,CPA.Nicodemus Mkama, akifurahia ahadi ya ushirikiano iliyotolewa na Prof. Mohamed Warsame, wakati wa utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la CMSA kwa Taasisi za Elimu ya Juu.
No comments:
Post a Comment