Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya WAJIBU imesema kuwa kuanzia Septemba 28 hadi 29 mwaka huu kutafanyika mkutano wa kimataifa wa uwazi na uwajibikaji ambao utafanyika jijini Arusha na wajumbe 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania watashiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU FCPA. Ludovick Utouh amesema Mkutano huu wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji (ITAC) ni wa tatu tangu WAJIBU ilivyoanza kuaanda mikutano ya aina hii mwaka 2021.
Amesema Mkutano wa ITAC utakuwa na maudhui isemayo; ‘‘Strengthening Accountability for Climate Action’’’ (Kuimarisha Uwajibikaji kwa Mabadiliko ya Tabianchi).
Ameongeza kuwa WAJIBU imeandaa mada mbalimbali zitakazowasilishwa na watoa mada wa ndani na nje ya nchi na mada hizo ni Sayansi ya Mabadiliko ya Tabianchi (The science of climate change), Ufadhili wa kifedha wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Mada nyingine ni Mbinu bora na changamoto katika kufuatilia mtiririko wa fedha za Mabadiliko ya Tabianchi ( The Climate Change Financing; Best practices and challenges in tracking and monitoring climate finance flows) pamoja na Vihatarishi vya kifedha katika Mabadiliko ya tabianchi (Climate change and fiscal risks).
Pia kutakuwa na mada ya Ushiriki wa sekta binafsi katika ufadhili wa kifedha wa mabadiliko ya tabianchi na taratibu za uwajibikaji wa fedha za sekta binafsi (Private sector engagement in climate change financing and the accountability mechanisms for private finance).
Aidha Mbinu Bunifu kwa ajili ya kukabiliana na kuendana na mabadiliko ya tabianchi (Innovative Mechanism for climate change Mitigation and adaptation)
"Kwa kuzingatia umuhimu wa maudhui ya mkutano huu WAJIBU inatarajia mkutano wa ITAC utahusisha washiriki kutoka taasisi za Serikali, wadau wa maendeleo, wanadiplomasia, wanaazaki, wabobezi wa masuala ya uwazi na uwajibikaji, wabobezi wa masuala ya mabadiliko ya Tabianchi, wanataaluma mbalimbali pamoja na wanahabari kutoka ndani na nje ya nchi.
" Ushiriki utakuwa wa aidha moja kwa moja (physical) au kwa njia ya mtandao (online) kupitia mitandao ya mawasiliano itakayochaguliwa. WAJIBU inatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 300 katika mkutano huo, "amesema FCPA Utouh.
Akieleza zaidi kuhusu mkutano huo amesema wanatarajia kuwa na mgeni rasmi ambaye ni mmoja wa viongozi wakubwa kitaifa nchini, ila kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu hatuwezi kumtaja hivi sasa.
Amesema wanategemea mkutano huo kuwa na watoa mada wa kimataifa ili kuleta ladha ya Kimataifa kwa kupata uzoefu wao kutoka katika nchi Sita ambazo ni mwenyeji mwenyewe Tanzania, Afrika ya Kusini, Kenya, Zimbabwe, Nigeria na Zambia.
" Na watoa mada kutoka katika nchi hizo wameshathibitisha ushiriki wao katika Mkutano huu mkubwa wa Kimataifa wa Uwajibikaji (ITAC 2023).Mkutano huo unatarajiwa kuleta uelewa mzuri juu ya changamoto na fursa zinazohusiana na uwajibikaji wa kifedha wa umma katika kugharamia hatua ya mabadiliko ya tabianchi, na kubainisha mikakati ya kuimarisha mifumo ya uwajibikaji wa kifedha."
Amefafanua washiriki watapata fursa ya kubadilishana ujuzi na uzoefu, usimamizi mzuri zaidi wa fedha zinazohusika na mabadilko ya tabianchi, kutambua vihatarishi (risk) vilivyopo na namna ya kushughulikiwa na kupanga wakati wa ushiriki wa pamoja kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi hayana mipaka.
Hivyo WAJIBU inatoa rai kwa wadau wote wa uwazi na uwajibikaji kutoka ndani na nje ya nchi kushiriki mkutano huo wa Kimataifa wa ITAC 2023 ambao ni fursa ya kujadili na kubadilishana mawazo ya nini kifanyike ili kukuza na kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwenye usimamizi wa fedha na rasilimali nyingi zinazohitajika kwenye kugharamia kudhibiti hali ya mabadiliko ya tabianchi kwa maendeleo ya nchi za bara la Afrika.
Aidha, watu wenye fani za Masuala ya Mazingira, uhasibu, uchumi, sheria, utafiti, waandishi wa Habari, wana geologia na maendeleo ya jamii, mkutano huo ni muhimu kwao kwani mada zitakazojadiliwa zinahusu moja kwa moja utendaji wa kazi zao.
Pia amesema wanashauri wadau wote kuanza kujiandikisha kushiriki kwenye Mkutano huu kupitia tovuti yetu ya www.wajibu.or.tz ambapo mwisho wa uandikishaji utakuwa tarehe 18/09/2023.
"Masharti ya ushiriki kwenye Mkutano huo kwa Washiriki wanaotokea nchini – (Residents) watakaohudhuria ukumbini – (physical) na watakaoshiriki kwa njia ya mtandao (online) kuchangia kidogo gharama za mkutano kwa malipo ya TZS 25,000/-.
"Washiriki wanaotokea nje ya nchi – (non-Residents) watakaohudhuria ukumbini – (physical) na watakaoshiriki kwa njia ya mtandao (online) kuchangia kidogo gharama za mkutano kwa malipo ya USD 15/-
"Akaunti ya washiriki waliopo nchini (Local Account): Jina la Benki: NMB Plc, Jina la Akaunti :WAJIBU – Institute of Public Accountability Akaunti Na:TZS 20110018487.Tunawaomba washiriki kuthibitisha ushiriki wao na kufanya malipo kabla ya tarehe 25/09/2023." amesema FCPA.Utouh.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya WAJIBU FCPA. Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Septemba 12,2023 kuhusu kufanyika mkutano wa tatu wa kimataifa wa uwazi na uwajibikaji (ITAC) ambao utafanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 28 hadi 29 mwaka huu,ambapo wajumbe 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki. Mkutano huo wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji (ITAC) ni wa tatu tangu WAJIBU ilivyoanza kuaanda mikutano ya aina hii mwaka 2021.Pichani kushoto ni Meneja Miradi Moses Kimaro.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya WAJIBU FCPA. Ludovick Utouh wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika mkutano wa tatu wa kimataifa wa uwazi na uwajibikaji (ITAC) ambao utafanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 28 hadi 29 mwaka huu,ambapo wajumbe 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki. Mkutano huo wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji (ITAC) ni wa tatu tangu WAJIBU ilivyoanza kuaanda mikutano ya aina hii mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment