HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 19, 2023

VETA:Mafundi wenye ujuzi wapo kutosha wa kutumika katika miradi ya ujenzi

*Wahandisi na Makandarasi wawatumie katika miradi

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema kuwa katika miradi ya ujenzi inayotekelezwa nchini  kwa  Wakandarasi kutumia mafundi wenye ujuzi ambao wamehitimu katika vyuo  vya VETA.

Hayo ameyasema Afisa Uhusiano wa VETA Dora Tesha kwenye Maonesho na Mkutano Mkuu wa 20 wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (ERB)yaliyofanyika Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Dora amesema  wahitimu wa VETA ni mafundi wenye ujuzi ambapo wanaweza kufanya kazi na kuwarahisishia  Wahandisi na Wakandarasi kuwa mafundi walionao wameiva.

Aidha amesema kuwa baadhi ya vijana waliohitimu VETA wako katika kampuni mbalimbali na mrejesho wake wa katika kazi ni mzuri na kutaka vijana waende katika vyuo vya VETA kupata ujuzi.

Amesema kuwa Vyuo vya VETA vimejengwa kila Wilaya ambapo vijana waende kupata mafunzo ya ufundi Stadi na ambao wanafanya kazi za ufundi bila kuwa na mafunzo VETA inachukua na kuwatambua kwa kuwapitisha programu maalumu ya Wanagenzi.

Mwanafunzi wa VETA Chang'ombe fani ya Fundi bomba Kebori Mwita amesema VETA ni mkombozi kwake kwani ana uhakika wa kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri kutokana mahitaji mafundi bomba.

Amesema kuwa vijana watumie fursa za mafunzo ya ufundi stadi kwani ni uhakika wa kupata kazi moja kwa moja ya kujiajiri ambapo haijawahi kutokea fundi akakosa kazi.

Kwa upande wa Mwanafunzi wa Chuo hicho Fani ya Useremala Nuru Ally amesema kuwa amechagua fani hiyo kutokana na kuipenda kwa kuamini itamsaidia katika ajira ya uhakika pia wasichana wa kike wanaikimbia hivyo yeye anafungua milango.

Afisa wa Chuo cha VETA Chang'ombe Anna Temu akizungumza na wateja waliootembelea banda la VETA katika maonesho ya Makandarasi jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Fani ya Ufundi Bomba Kebori Mwita akizungumza fani ya Fani hiyo kwenye fursa ya ajira kwenye maonesho na Mkutano Mkuu wa 20 wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (ERB) jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa VETA Dora Tesha akizungumza na waandishi wakati wa maonesho na mkutano wa 20 wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi uliofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad