HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 14, 2023

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WAJUMBE WA KAMATI ZA SERIKALI ZA MTAA

MTANDAO wa Kijinsia Tanzania TGNP imeendesha Mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati za Serikali za Mitaa katika kuwajengea uwezo juu ya masuala ya uwezeshaji wa Wanawake katika nafasi za uongozi.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mwezeshaji Bi.Mary Msemwa amesema kupitia mafunzo hayo tutegemee ushiriki wa wanawake katika ngazi ya maamuzi wataimarika.

Aidha amesema wanawake waliopo kwenye ngazi za maamuzi ni wachache hivyo kupitia mafunzo hayo yatawajengea uwezo na uthubutu kugombea nafasi za uingozi kwenye uchaguzi ujao.

Kwa upande wa washiriki wamesema kuwa katika Kamati zao kumekuwa na changamoto ya usawa wa kijinsia hsa kwneye kamati za ulinzi na usalama ambapo wanaume wengi wapo kwenye kamati hiyo kuliko wanawake kutokana wengi kuamini ya kuwa kazi hiyo hufanywa na wanaume tu.

Nae Mjumbe wa Kamati ya Serikali ya Mtaa wa Kivule Bw.Erick Anderson amesema kupitia Mafunzo hayo wanakwenda kuboresha zaidi kwenye kamati zao ili waweze kupata maendeleo endelevu.

Amesema watatumia Mafunzo hayo kwenda kutoa elimu ya usawa wa kijinsia katika Kamati zao katika kuhakikisha jamii inafanya maendeleo makubwa hasa kutokana na uwepo wa usawa wa kijinsia.

Amesema mafunzo hayo yatakwenda kusaidia kufanya maboresho zaidi katika Kamati zao ili waweze kupata Maendeleo endelevu.












No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad