TAASISI ya Kilimo hai nchini (TOAM) imepanga kuzindua mkakati wa kilimo hai wenye kuhimiza umuhimu wa kutunza asili kwa ajili ya uendelevu wa afya na mazingira na kuboresha mnyororo mzima wa kilimo kuanzia uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Mtendaji Mkuu wa TOAM, Bakari Mongo amesema hayo leo wakati akizungumzia kufanyika Kwa mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo hai (NEOAC) unaotarajiwa kufanyika Novemba 8 Hadi 9,2023 mkoani Dodoma ukishirikisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali.
Ameeleza kuwa mkakati huo ambao utazinduliwa wakati wa mkutano huo unawalenga wazalishaji kuwa na kilimo endelevu lakini pia ukiangalia suala la afya ya udongo na mbegu kwa ujumla.
Mongo amesema pia watatumia mkutano huo kuongeza washiriki kutoka taasisi na mashirika mbalimbali.
"Mkutano huo una kauli mbiu ya kutunza vya asili kwa afya bora, ambayo inalenga kuchochea juhudi na mchakato wa kuhamisha kilimo hai kufikia kwenye matokeo katika ngazi ya nchi," amesisitiza.
Mongo amesema wadau wa kilimo watatoa uzoefu wao, changamoto na simulizi za mafanikio katika kukuza uelewa na ushirikiano.
Kuhusu ushiriki wa kilimo hai kwenye miradi ya kilimo nchini, Mwenyekiti wa Kilimo hai Tanzania, Dkt Mwatima Juma ameshauri serikali kutenga kiwango cha fedha ili kilimo hai kuwezesha kutekelezwa nchini.
Amesema katika mradi wa BBT, iwapo serikali ina fedha za utekelezaj ione umuhimu wa kuwezesha kilimo hicho lakini pia upande mwingine wao waelimishe kuhusu kilimo hai.
"Kama serikali imekiri kuwa inazo fedha dola za Marekani milioni 160, kwa ajili ya BBT ione umuhimu wa kutenga hata Dola 1,000 kwa ajili ya wadau kutekeleza mradi wa kilimo hai," amesema Dkt. Mwatima.
Amesema kilimo hai sio suala la wakulima pekee bali pia ni la walaji ili waweze kusema wanachokitaka kwamba watumie mazao yenye msingi wa afya zao.
Ameshauri serikali pia kusaidia kutoa elimu zaidi ya jilimo hai kwani inaimarisha afya na kutunza mazingira pia.
Mtendaji Mkuu wa Toam, Bakari Mongo, akizungumza na waandishi wa habari wakati akItangaza juu ya uwepo wa mkutano wa tatu wa kitaifa wa Kilimo Hai ( NEOAC) utakaofanyika Novemba 8 hadi 9, 2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TOAM Tanzania na mjumbe wa kamati ya kumshauri Rais kwenye uhakika wa chakula nchini Dkt. Mwatima Juma, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya kilimo hai wakati wa kutangazwa kwa mkutano wa tatu wa kitaifa wa Kilimo Hai ( NEOAC) utakaofanyika Novemba 8 hadi 9, 2023 jijini Dodoma
Mtendaji Mkuu wa Toam, Bakari Mongo, akizungumza na waandishi wa habari wakati akItangaza juu ya uwepo wa mkutano wa tatu wa kitaifa wa Kilimo Hai ( NEOAC) utakaofanyika Novemba 8 hadi 9, 2023 jijini Dodoma, Kulia kwake ni Charles Bupambe mjasiliamali kutoka Kilimo Hai na Abdallah Ramadhani, mratibu kutoka Tabio.
Abdallah Ramadhani akizungumza wakati wa kikao hicho.
No comments:
Post a Comment