Uko tayari kushiriki kwenye NCBA Golf Series ya mwaka 2023? Basi muda wa kufanya hivyo umefika kwani tayari mashindano haya makubwa yamefika Tanzania. Ikiwa yamepangwa kufanyika siku ya Jumamosi, tarehe 30/09/2023 mashindano haya yanatarajiwa kuwa yenye msisimko wa hali ya juu kwa wapenzi wa mchezo huu nchini Tanzania.
Mashindano haya yatajumuisha wachezaji kutoka maeneo mabalimbali nchini Tanzania walioalikwa na Benki ya NCBA. Wachezaji hawa watakuwa wakiwania nafasi tatu za kwenda kushiriki fainali ya mashindano haya Nairobi, Kenya.
Safari ya mashindano haya mwaka huu imepita katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na sasa Tanzania kisha fainali ya mwisho itafanyika Nairobi, Kenya kuwapata washindi wa jumla wa mashindano haya makubwa.
Kinachofanya mashindano haya kuwa ya kipekee zaidi ni nafasi inayowapatia washindi. Kutakuwa na makundi matatu ya mabingwa: mshindi wa jumla, mshindi wa jumla kwa wanaume, na mshindi wa jumla kwa wanawake. Safari ya mabingwa hawa haitaishia kwenye viwanja vya Gymkhana Club badala yake watasafiri kwenda Nairobi, Kenya kuungana na mabingwa wengine kwa ajili ya kuwapata mabingwa wa jumla wa NCBA Golf Series ya mwaka 2023.
Safari hii ya kuelekea Nairobi italipiwa kila kitu na Benki ya NCBA hivyo kufanya ushindi kwa mabingwa wa Tanzania kuwa na ladha zaidi. Nchini Kenya, wataungana na washindi wengine kutoka maeneo mbalimbali katika mchuano wa mwisho kubaini washindi wa jumla wa mashindano yote ambapo washindi watatu, mmoja kutoka kila kundi, watapokea KSH 100,000.
NCBA Golf Series si tu kuhusu ushindani; ni juu ya kuimarisha hisia za urafiki na upendo kwa mchezo huu miongoni mwa wadau wake katika eneo la Afrika Mashariki. Mashindano haya yanakutanisha wachezaji wa golf na mashabiki, yakiumba nyakati za kumbukumbu ambazo zinaimarisha uhusiano kati ya Benki ya NCBA na wateja wetu wenye thamani.
Hivyo basi, weka katika kumbukumbu zako Jumamosi, Septemba 30, 2023, na jitayarishe kuona vipaji vikubwa vya golf vikionyeshwa pale Gymkhana Golf Club.
No comments:
Post a Comment