Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Shirika la GFP International kujenga karakana ya umahiri ya Uchomeleaji Chuo cha Ufundi Don Bosco Jijini Dar es Salaam.
Kujengwa Karakana hiyo itakuwa ndio Karakana ya kwanza kwa Afrika Mashariki ambapo vyeti vikitolewa katika chuo hicho vitambulika Kimataifa.
Akizungumza wakati sherehe za kujengwa Karakana hiyo katika Chuo cha Don Bosco Mwasisi wa GFP International Michael Vallez amesema kuwa ujenzi wa huo utazingatia viwango vya kimataifa na walimu ambao watakwenda kusoma umahiri nchini Afrika Kusini ndio watakuwa Walimu katika Karakana hiyo ya Kisasa.
Amesema kuwa fani ya uchomeleaji iko katika sekta nyeti za mafuta na Gesi ambapo wanaofanya kazi hiyo lazima wawe na vyeti vya Kimataifa vya kuweza kuomba kandarasi kwenye sekta hiyo.
Vallez amesema kuwa umahiri katika uchomeleaji ndio unahitajika kwani kampuni nyingi zinahitaji kuwa na wakandarasi wenye viwango vya kimataifa.
Mkurugenzi Mkazi wa GFP International Hilu Bura amesema kuwa dunia imebadilika wenye ujuzi na ufundi wanahitaji kuendeleza katika viwango vya kimataifa.
Bura amesema kuwa Tanzania tumebarikiwa kujengewa chuo cha umahiri hivyo kitapoanza chuo watu wasome na wasiposoma watakuja watu kutoka nchi nyingine watasoma na miradi mikubwa watakuwa wao ndio wenye sifa za kufanya.
Bura amesema ni bahati kupata watu wa kuwasomesha nje ya nchi hivyo wanaokwenda wakazingatie ili kuleta tija kwenye Taifa.
Mwalimu wa Uchomeleaji wa Don Bosco Erick Nkula amesema kuwa wanategemea kuzalisha watu wengi na nje ya nchi.
Amesema Don Bosco kujengwa kwa Chuo hicho watakuwa wametimiza ndoto watakwenda mbali huku mahitaji yataongezeka katika udahili.
Amesema kuwa katika ujenzi wa karakana ya umahiri utaendana na vifaa ambavyo vinatambulika kimataifa na hata ujenzi wa jengo ni kutambulika Kimataifa.
Mwalimu wa Uchomeleaji wa Chuo cha Don Bosco Erick Nkula akizungumza faida ya ujenzi wa karakana ya kisasa ya uchomeleaji katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mwasisi wa GFP International Michael Vallez akiwa na baadhi ya watendaji wa GFP wakiwa na majembe kuashiria sehemu itakayojengwa Karakana ya Umahiri ya Uchomeleaji Don Bosco, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi GFP International Hilu Bura akizungumza kuhusina juu ya faida ya umahiri wa kutambulika kimataifa katika Uchomeleaji , jijini Dar es Salaam.
Mwasisi wa GFP International Michael Vallez akizungumza katika Chuo cha Don Bisco kuhusiana Ujenzi wa Karakana ya Kisasa ya Kisasa ya Uchomeleaji itakayotambulika Kimataifa, jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment