MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya maarufu Bongo Fleva Nassib Abdull a.k.a Diamond Platnumz ameungana na Kampuni ya SBC Tanzania wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Chupa mpya ya Pepsi iliyopewa jina la Mwamba wao.
Wakati wa uzinduzi huo Diamond ambaye ni Balozi wa kinywaji cha Pepsi amewaomba Watanzania kuendelea kuburudika na Pepsi Mwamba wao huku akisisitiza kwa Tanzania Pepsi ndicho kinywaji kinachopendwa zaidi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Diamond amesema Chupa ya Pepsi Mwamba Wao imeingia sokoni ikiwa na ujazo wa mililita 350.
"Niwashukuru sana Pepsi katika kipindi cha miaka mitano tumekuwa tukifanya kazi pamoja , nikiwa kama mwanamuziki kitu chochote nachoshirikiana nacho kisipofanya vizuri kwangu mimi najua inaniharibia hata 'karia' yangu..
"Lakini partna ni watu sahihi hawajaniangusha na sio wao tu lakini na wateja wetu, washabiki, wadau kila mmoja amekuwa akihakikisha Pepsi ndio inakuwa kinywaji namba moja nchini
"Ni heshima kubwa kwangu, kwa Partna zangu ambao nashirikiana nao na kwasababu hiyo tumekuja na kampeni mpya ya Chupa yetu mpya yenye ujazo wa mililita 350 inayoitwa Mwamba Wao.
" Kama alivyosema kiongozi wangu kwanini tunaita Mwamba Wao kwasababu katika kipindi chote Pepsi imeendelea kutawala na kuwa kinywaji namba moja."
Diamond amesema kuna watu ambao wamekuwa wanakuja nchini na wakifika huwa wanauliza vinywaji vingine nchi hii hakuna."Wanauliza kwasababu wanachoona sokoni ni Pepsi.Wengine wanauza lakini kwa bahati mbaya kwani hawana bahati ya kukubalika na kupendwa kama ilivyo sisi.
Amewapongeza Pepsi kwani inapofika wakati wa kufanya promosheni hawana jambo dogo na hata yeye anasikia raha na wala hana wasiwasi."Wenzetu wa mtaani sasa tumeleta mililita 350 ,mtu anachukua anakunywa anachukua nyingine.
Kwa upande wake Meneja Masoko kutoka Kampuni ya SBC Tanzania Limited Jasper Maston amesema wameweza kumfanya Diamond kuwa sehemu ya familia ya Pepsi na wamekuwa wakishirikiana katika mambo mbalimbali ya biashara na masoko.
"Kupitia uwezo wa Diamond Platnuz tumeweza kutawala jukwaa la muziki wa Tanzania kitu ambacho kimesababisha wote kuwa na mafanikio katika kazi zetu tunazofanya.Katika kuadhimisha miaka mitano leo hii tunazindua kampeni ya Chupa yetu Pepsi ya Mililita 350
"Chupa hii tumeweza kuipa jina ambalo linatumika sokoni kulingana na balozi wetu Diamond Platnumz na wakati huo huo tunategemea zaidi kumpa nafasi ya kuburudisha Watanzania wengi zaidi wateja wa Pepsi na ambao sio kuwaleta kwa upande wetu waweze kufaidika na bidhaa yetu
"Chupa hii ya Peps tumeipa jina la Mwamba Wao , kimsingi kwanini tumeita jina la Mwamba Wao kwasababu katika miaka hii mitano tumeweza kufanya kazi pamoja , tumesimika Chapa hii ya Pepsi kuweza kuwa Mwamba Wao .
Wednesday, September 27, 2023
DIAMOND PLATNUMZ AFURAHIA PEPSI 'MWAMBA WAO KUINGIA' SOKONI KIBABE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment