Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Mobhare Matinyi (katikati) Sheikh wa Kata ya Kiburugwa Said Kiduka na Mhe. Diwani wa Kata hiyo Fatma Shija wakiwa na wakandarasi wa usafi wa kata ya Kiburugwa.
Kushoto ni Mh.Diwani Kata ya Kiburugwa Fatma Shija Sheikh wa Kata hiyo Said Kiduka na Mhe.Mobhare Matinyi wakifanya usafi
DC Matinyi akielekeza jambo wakati wakikagua nyumba ambazo hupata mafuriko.
Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mhe. Mobhare Matinyi leo Septemba 23, 2023 ameungana na wananchi wa Kata ya Kiburugwa katika Tarafa ya Mbagala Wilayani Temeke Mkoani Dar es Salaam kufanya usafi katika Zahanati ya Kingugi.
Zoezi hilo la usafi limeandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika Kata ya Kiburugwa na kuongozwa na Sheikh Saidi Kiduka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Maulid ya Mtume Muhammad (SAW).
Akizungumza mara baada ya usafi huo na kuwashukuru uongozi wa BAKWATA, Zahanati, Kata, Mtaa na wananchi kwa ujumla Mhe. Matinyi amesema "Ndugu wananchi tuendelee kufanya usafi kwa ajili ya mazingira yetu na afya zetu na zoezi hili liwe endelevu."
Sheikh Kiduka amesema kuwa usafi ni jambo muhimu katika jamii ambalo hata Mtume Muhammad
(S.A.W) alilisisitizia na kumnukuu katika maneno yake akisema kwamba 'Al Islam nadhwiif akimaanisha kuwa Uislamu ni usafi".
Diwani wa Kata hiyo Mhe. Fatma Shija ameshiriki katika zoezi hilo huku akiambatana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa ngazi ya Kata na Mtaa na hali kadhalika Wenyeviti na Watendaji wa Kata na Mitaa.
Baada ya zoezi hilo Diwani Shija alimchukua Mhe. Matinyi katika ziara fupi kumwonesha changamoto za miundombinu ya barabara mifereji na mitaro katika Kata hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya ya Temeke amesema kuwa amejionea mwenyewe na amezipokea changamoto hizo.
No comments:
Post a Comment