HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 20, 2023

Benki ya Absa yasogeza karibu huduma za kibenki kwa watanzania ikizindua Absa Wakala

 

 Benki ya Absa Tanzania imezindua huduma yake ya Absa Wakala ikiwa ni mikakati ya benki hiyo katika kusogeza huduma za kibenki karibu na watanzania sambamba na lengo lake la kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja - hatua moja baada ya nyingine.


Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bwana Obedi Laiser alisema uzinduzi wa Absa Wakala utasaidia kwa kiasi kikubwa juhudi za serikali katika azma yake ya kufikisha huduma za kifedha karibu zaidi na kwa watanzania wengi zaidi hususan katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za kiasili za kifedha.


Bwana Laiser alisema “Dhumuni la Benki ya Absa Tanzania ni kuunga mkono ajenda ya serikali ya kutoa huduma za kifedha kwa wananchi wote, Absa Wakala tunayozindua leo itakuwa suluhu na itachangia zaidi ujumuishwaji kwa kifedha nchini, Benki ya Absa Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa pengo la watu wasiopata huduma za benki nchini linapungua hususani kwa wakazi wa vijijini.


“Nina furaha kubwa sana kuwashirikisha hatua nyingine muhimu ambayo benki yetu ya Absa imefikia leo hii kuzindua huduma ya Absa Wakala, hatua hii muhimu ni katika jitihada zetu za kufikia lengo letu kuu la shirika, ambalo ni kuwezesha Afrika ya kesho, pamoja - hatua moja baada ya nyingine.

“Kama mnavyofahamu, Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi zinazohusiana na upatikanaji wa huduma za kifedha, jambo linalothibitishwa na viwango vya chini vya ushirikishwaji wa kifedha nchini Tanzania, msongamano wa benki nyingi katika miji mikubwa/miji yenye mzunguko mkubwa wa biashara, muda mdogo wa kufanya kazi kwa benki za biashara, ni baadhi ya changamoto ambazo zimechangia idadi kubwa ya watu kutofikiwa na huduma za benki nchini.

“Huduma ya Kibenki ya Absa Wakala (Absa Wakala) tunayoizindua leo ni mojawapo ya chaneli zitakazotoa suluhu kwa baadhi ya changamoto hizo na kusaidia kwa kiasi kikubwa Bara la Afrika kuondokana na baadhi ya changamoto za kiuchumi na za kijamii,” anasema Bwana Laiser.

Mkurugeni huyo aliongeza kuwa kupitia Absa Wakala, hakutakuwa na haja tena ya wateja kusafiri umbali hadi benki, hakutakuwa na kusimama kwenye foleni ya benki, na shughuli za malipo zitafanyika kwa uharaka zaidi. Aidha, huduma hiyo ni nafuu kwa mwananchi wa kawaida, kwani ada za miamala zitakuwa chini kuliko zile za matawi na pia muda wa kupata huduma pia utaongezeka, kwani mawakala hufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko matawi, na huduma zitakuwa rahisi zaidi bila kuhitaji kujaza fomu nyingi.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa, Bi. Ndabu Lilian Swere alisema uzinduzi wa Absa Wakala ni ushahidi mwingine wa jinsi benki hiyo ilivyojizatiti katika kutimiza ahadi zake za kusogeza huduma karibu kwa watanzania na tena kwa kutumia njia rahisi na nafuu.

“Kwa kuonyesha tunawajali wateja wetu mara baada ya uzinduzi huu kwa muda wa miezi miwili wateja watakaokwenda kufanya miamala kwa mawakala wetu wataweza kupata huduma bila ada yoyote,” alisema Bi. Ndabu.

Akizungumzia baadhi ya huduma zitakazopatikana kwa wakala wa Absa, Mkuu wa Mikakati na Bidhaa Rejareja wa Absa, Bwana Heristraton Genesis alizitaja baadjhi ya huduma kama kutoa pesa kwa kutumia Kadi, kuweka pesa kwenye akunti kwa kutumia kadi, kupata taarifa fupi za akaunti ya benki, kuangalia salio la akaunti ya benki pamoja na kutuma pesa kwa kadi (Absa kwenda Absa).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (wa pili kushoto), akiwa na baadhi ya maofisa wa benki hiyo kutoka kushoto; Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bwana Aron Luhanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja, Bi. Ndabu Lilian Swere na Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Rejareja, Bwana Heristraton Genesis, wakizindua rasmi huduma za kifedha za Absa Wakala, jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Huduma ya Absa Wakala, jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bwana Aron Luhanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere na Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Rejareja, Bwana Heristraton Genesis

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (wa pili kulia), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Huduma ya Absa Wakala, jijini Dar es Salaam jana. Pamoja naye kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bwana Aron Luhanga, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bwana Obedi Laiser na Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Rejareja, Bwana Heristraton Genesis

Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Rejareja wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Heristraton Genesis (kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu huduma za Absa Wakala katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni; Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Lilian Swere, Mkurugenzi Mtendaji, Bwana Obedi Laiser na Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bwana Arona Luhanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (wa pili kushoto, waliokaa), akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati Absa Tanzania ikizindua huduma zake za kibenki kwa kutumia Absa Wakala.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad