WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amekutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ajili ya kujitambulisha na kufanya naye mazungumzo.
Profesa Mkumbo amekwenda kujitambulisha ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza la mawaziri na kuunda Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na kisha kumteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa waziri wake na Dkt. Tausi Kida kuwa Katibu Mkuu.
Pamoja na kukutana na Rais Mwinyi, Prof. Mkumbo pia amekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Zanzibar Mudrik Soraga, ambapo katika mazungumzo yao, kwa pamoja wamesisiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kwatika kukuza uwekezaji ili kukuza uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla.
Pro. Mkumbo pamoja na ujumbe wake wamepata nafasi ya kutembelea eneo la uwekezaji wa bandari kubwa inayojengwa Zanzibar eneo la Mangapwani.
Ujumbe ulioongozana na Waziri Prof.Kitila ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dk.Tausi Kida, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mkuu EPZA Charles Itembe, Mkurugenzi Mkuu TIC Gilead Teri, Mkurugenzi wa Miundombinu wa Mamlaka ya Bandari Dkt.Hussein Lufunyo Wakurugenzi wa Wizara.
No comments:
Post a Comment