Mwalimu wa VETA Kihonda William Munuo akizungumza na madereva mara baada ya kuhitimisha mafunzo katika kampuni ya WorldOil Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
*Madereva wapongeza mafunzo kwa kampuni kuchukua Mwalimu wa VETA Kihonda
Na Chalila Kibuda , Michuzi TV
CHUO cha VETA Kihonda Kimetoa mafunzo kwa madereva wa kampuni ya WorldOil jijini Dar es Salaam ikiwa madereva kuwa udereva wa kujihami wakati pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani.
Akizungumza mara baada ya mafunzo ya wiki mbili Mwalimu wa VETA Kihonda William Munuo amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa usalama wa barabarani pamoja na kupata elimu ya Teknolojia ya magari yanayobadilika kila wakati .
Amesema kuwa VETA Kihonda imebobea kwa udereva wa magari makubwa hivyo umekuwa ni utaratibu wa kwenda katika kampuni mbalimbali kutoa elimu ya udereva.
Munuo amesema kukiwepo kwa madereva wenye mafunzo makosa ya kibindamu yanapungua kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na madereva wasio na mafunzo.
Aidha amesema kuwa licha ya kuwepo na mafunzo hayo amesema magari makubwa kwa teknolojia ya sasa yana umeme mwingi pamoja na upepo hivyo mafunzo kwa madereva ni muhimu.
"VETA kazi yenu ni kufikisha elimu kwa ajili ya madereva ambayo ndio kazi yetu kubwa katika kufanya madereva wasio na ajali ambapo Taifa ndio linapunguza nguvu kazi" amesema Munuo.
Mwalimu wa mafunzo wa WorldOil Saimon Majeni amesema kuwa mafunzo waliyopata kutoka Kihonda inaongeza tija kwenye kwenye kampuni na kuahidi kuendelea na ushirikiano wa mafunzo ya mara kwa mara.
Amesema kampuni hiyo ina magari zaidi 300 katika uwanja wao hakuna hata gari moja lenye ajali hali inaonyesha madereva wanapata mafunzo na kuyafanyia kazi.
Fundi Mkuu wa Worldoil Hassan Kasagamba amesema kuwa dereva akiwa na mafunzo hata tatizo la gari anaweza kujieleza katika kufanya matengenezo kuliko wasio na mafunzo hawaelewi tatizo la gari lilipoanzia.
Dereva Mbwana Muchuzi amesema kuwa mafunzo wanashukuru mwalimu pamoja na Menejimenti ya Worldoil kuwapelekea mafunzo.
Madeva wakiwa na furaha mara baada ya mafunzo kuhitimishwa katika kampuni ya WorldOil jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa mafunzo wa Worldoil Saimon Majeni akizungumza umuhimu wa mafunzo yaliyotolewa na Chuo cha VETA Kihonda jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya madereva wakiwa darasa la nadharia ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya Udereva katika kampuni ya WorldOil jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment