HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 24, 2023

TRA YAZAINDUA KAMPENI UHAMASISHAJI MATUMIZI SAHIHI YA RISITI ZA EFD

 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MENEJA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kinondoni mkoani Dar es Salaam Husna Nyange amesema kodi sahihi inatokana na kumbukumbu sahihi za kikodi hivyo amewahimiza wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapofanya mauzo.

Pia na wanunuzi kudai risiti sahihi za EFD kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma lengo likiwa kila mmoja kwa nafasi yake anatunza kumbukumbu zake.

Nyange ameyasema hayo leo Agosti 24, 2023 wakati wa uzinduzi wa mabango ya uhamasishaji kuhusu matumizi sahihi ya EFD

Hivyo pamoja na mambo mengine ameelezea umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na kumbukumbu sahihi za kikodi hivyo lakini wanunuzi nao ni vema wakajenga utamaduni wa kudai risiti kutoka kwa wafanyabiashara.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Mlipakodi Mkoa wa kikodi Kinondoni Emanuel Lucian Dafay amesema kampeni hiyo ya EFD ni endelevu na kwa mkoa wa Kinondoni walianza kwa kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa wafanyabiashara kupitia simu zao za mkoni.

Amefafanu lengo la kutuma ujumbe ili kuwakumbusha kuhusu wajibu wao wa kutoa risiti sahihi za EFD.“Wafanyabiashara wa Mkoa wetu wa Kinondoni wamepata meseji za kuwakumbusha umuhimu wa kutoa risiti, "amesema.

Wakati huo huo wafanyabiashara wameipongeza TRA kwa kuendelea kuwakumbusha wajibu wao kuhusu mambo mbalimbali ya kikodi ikiwemo kutoa na kudai risiti.

Pia wafanyabiashara wamehaidi kutimiza wajibu wao wa kutoa risiti kila watakapofanya mauzo.






1 comment:

  1. Kazi nzuri sana. Na sisi wafanyabiashara tuwaunge mkono TRA kwa kutoa risiti sahihi. Haina haja ya kusukumana na serikali kila mara. Tutoe risiti, na huo ndo uwajibikaji.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad