KITUO cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimefanya kikao na viongozi wa Jumuiya za wanawake wa vyama wanachama wa TCD kujadili namna ya kuanzisha jukwaa la wanawake chini ya Kituo hicho.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Kituo cha Demokrasia Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Agosti 09, 2023 huku vyama; CHADEMA, CCM, CUF, ACT-WAZALENDO pamoja na NCCR - Mageuzi wakishiriki.
CHAUMMA wameshiriki kuwakilisha vyama visivyo na wabunge/madiwani.
Jukwaa hilo linaundwa ili kuwakutanisha pamoja viongozi wa Jumuiya za wanawake za vyama wanachama wa TCD kujadili masuala mbalimbali yanayolenga kutatua changamoto za wanawake katika siasa na uongozi.
No comments:
Post a Comment