HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 16, 2023

TAKUKURU PWANI YABAINI UKIUKWAJI WA MCHAKATO WA MANUNUZI KUMPATA MZABUNI

 Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani Christopher Myava akizungumza katika mkutano na na waandishi wa habari hawapo pichani uliofanyika leo Agosti 16, 2023 Ofisini kwake Kibaha.


Baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Kamanda Myava wakati akisoma ripoti ya TAKUKURU leo ofisini kwake.

Na Khadija Kalili Michuzi Tv 
KAMANDA wa  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani Christopher  Myava amesema  kuwa  wamegundua kuwa  baadhi ya wazabuni   wamepewa  kazi na Afisa  Manunuzi  wa Halmashauri  pasipo  kuomba kazi  hizo  kwa kupitia  mfumo wa manunuzi  ya umma yaani TANEPs.

"Hatua hii  imesababisha  wazabuni  kupata kazi  bila kufuata taratibu   za manunuzi ya umma   mfano  mzabuni  aliyechaguliwa  kuleta vifaa  vya ujenzi  katika  shule   mpya ya Sekondari  ya Kata ya  Shungubweni  iliyoko Wilaya ya  Mkuranga  hakuomba  kazi hiyo  kwenye mfumo wa  wa TANEPs na badala  yake amepatiwa zabuni na Afisa  Manunuzi  wa Halmashauri kinyume  cha utaratibu" Amesema  Kamanda wa TAKUKURU  Pwani Myava  

"TAKUKURU  Mkoa wa Pwani  tumegundua  uwepo wa Kamati  hewa  kwa baadhi ya  miradi  inayosimamiwa  na Halmashauri  jambo limesababisha uwepo wa  mianya ya rushwa  katika malipo yanayofanyika, jamii kutokuwa na umiliki wa miradi hiyo  kutokana na kutokusbirikishwa  katika utekelezaji  wake, mfano ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiju  hamii haikushirikishwa  kabisa katika   yaimamizi na utekelezaji wa  mradi huu" amesema Kamanda Myava.

Aidha TAKUKURU  wamebaini mianya ya  ukosefu wa uaminifu katika kukusanya ushuru  na usimamizi  uendeshaji  wa soko la Mnarani  Halmashauri ya Mji Kibaha   imebainika kuwa wakusanyaji  wa ushuru  kutotoa   risiti  za mashine ya POS  baada  ya wafanyabiashara  kufanya malipo kwa kisingizio cha   cha ubovu  wa mashine  au mashine kutokuwa na 'Charge'  jambo ambalo limesababisha  wakusanyaji  kutumia fedha  hizo kwa matumizi yao binafsi  na kusababisha  kukosekana kumbukumbu za wafanyabiashara waliofanya malipo yao" amesema Kamanda Myava.

"Upotevu  wa mapato ya maegesho unasababishwa  na utendaji mdogo  wa wakusanya  mapato ambapo  baadhi ya wakusanyaji  hutoza viwango  tofauti vya ushuru  wa malori  yanayoegesha  sokoni tofauti na viwango vilivyowekwa  kwenye sheria ndogo" amesema Kamanda Myava.

Kamanda  Myava amesema tayari wamekaa kikao na wadau wa soko la Mnarani  na kuweka maazimio moja wapo likiwa kukusanya mashine zote ambazo zinadaiwa kuwa mbovu ili kudhibiti huo mwanya,  wafanyabiashara wamepewa elimu  ili.kuhakikisha wanadai risiti  baada ya kufanya malipo ya ada na ushuru na kutakiwa kutoa taarifa  pindi wanapoelezwa na wakusanya ushuru kuwa mashine zA POS ni mbovu  ili kudhibiti upotevu wa  mapato yanayokusanywa".

Pia wamekubaliana kutengeneza vibao vitakavyo onesha  bei za tozo za maegesho ili kuepusha  kutoza viwango tofauti hususani kwa kila lori  linapoegeshwa sokoni kwa ajili ya kushusha bidhaa.

Kamanda   wa TAKUKURU  Mkoa wa Pwani  Myava amesema hayo leo Agosti 16  alipozungumza na Waandishi wa Habari  kwenye Mkutano uliofanyika ofisini kwake Kibaha  " Kipindi  cha robo  ya Aprili hadi Juni  2023,Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa  Mkoa wa Pwani  tumeendelea  na majukumu  yetu  katika  maeneo  ya uzuiaji rushwa ,uchunguzi pamoja na uelimishaji" amesema.


Amesema kuwa uchunguzi umefanyika wa tuhuma mbalimbali huku tayari kesi imefunguliwa Mahakamani  dhidi ya Afisa  Manunuzi  wa Halmashauri  ya  Mkuranga .

Amesema kuwa katika eneo la  uzuiaji rushwa  wamefanya ufuatiliaji miradi 11 ya  maendeleo yenye thamani ya  Shilingi.Bilioni  mbili milioni mia tatu  na  mbili na laki tano  hamsini na mia nne  ishirini na sita (2,302, 550,426/-) katika sekta za  elimu, afya, maji    barabara , masoko  na amendeleo ya jamii, katika  ufuatiliaji  wa utekelezaji wa miradi hiyo hakukuwa na  mapungufu yaliyobainika  katika miradi  hiyo iliyofanyiwa ufuatiliaji.

Ili kudhibiti mianya ya  rushwa katika  Idara  za serikali  na sekta  binafsi  tumefanya mikutano  ya hadhara 36,  semina nane  kwa watumishi  wa  serikali  na sekta binafsi imefanyika,maonesho nane yamefanyika,.klabu za wapinga  rushwa 96 zimeimarishwa  kwenye shule  za msingi na sekondari na elimu dhidi ya rushwq  imetolewa  kupitia vipindi bitatu vya redio.

Amesema  kuwa idadi ya malalamiko yaliyopokelewa ni 87,malalamiko  yanayohusu rushwa  62, yasiyohusu rushwa 25, malalamiko  yaliyohamishiwa  Idara  nyingine 04, yaliyoshauriwa 18  na yaliyofungwa hakuna.

TAKUKURU Mkoa wa Pwani imeweka mikakati yake katika kipindi cha  Julai hadi Septemba 2023 kuwa ni kiendeleza programu ya TAKUKURU Rafiki, kuendelea  kufanya  ufuatiliaji na chambuzi  za mifumo kwa lengo  la kuziba  mianya  ya rushwa  itakayobainika kuendelea  kukagua  utekelezaji  wa miradi yote  ya maendeleo ndani ya Mkoa wa Pwani.

Kuendelea kuelimisha umma wa watanzania  juu ya madhara  ya rushwa ili wafahamu nafasi yao katika  mapambano  dhidi  ya rushwa  kwa makundi yote katika jamii kuendelea  nauchunguzi  wa vitendo vya rushwa  na kuchukua  hatua  za kisheria  dhidi  ya wale  watakaobainika  kutenda makosa ya rushwa.

Kamanda wa TAKUKURU Pwani Myava ametoa wito  na kuwahamasisha wananchi na wadau  wote katika Taasisi za serikali  na sekta binafsi  kuendelea  kuunga mkono  juhudi za mapambano  dhidi ya rushwa  kwa kukataa kujihusisha  na vitendo  vya rushwa ,kufuatilia miradi  ya maendeleo  inayotekelezwa   kwenye maeneo  yao ili thamani ya fedha ya serikali  ionekane  na kwakufanya hivyo  miradi ya maendeleo  itatekelezwa  kwa kiwango kilichokusudiwa  na hivyo kuleta  maendeleo  na huduma bora  kwa wananchi, pia wananchi wanaombwa kutoa taarifa  za vitendo  vya rushwa  endapo utavishuhudia  au kusikia  ili wahusika  wachukuliwe hatua za kisheria 'Kuzuia rushwa  ni jukumu lako na langu, tutimize  wajibu  wetu' 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad